Sikuwahi kujua kama Mwalimu alipata mapokezi makubwa kiasi hiki WH. Dah!
Mkuu nimeona hii Video hakuna shaka kujiridhisha kuwa Tanganyika ya Nyerere ilikuwa inachukuliwa kama the great power.Ukizingatia mchango wake mkubwa katika kuleta uhuru wa mataifa Mengine ya Afrika,Viva Mwl Nyerere huko uliko.
Mimi nilisoma maandishi mpaka nikawa na shaka kama ni Nyerere kweli.Shukrani Mkuu kuna moja nimeona mahali nimeitafuta sana utube lakini sijafanikiwa. Inahusu kutwambia Watanzania tusiwe waoga kuwakabili madikteta watakaokuwa madarakani. Kwa hali ya nchi yetu ilivyo sasa utadhani Mwalimu aliliona hilo la kutawaliwa na dikteta. Hiyo ya FB nikiiweka hapa wengi hawataweza kuifungua.
Mimi nilisoma maandishi mpaka nikawa na shaka kama ni Nyerere kweli.
Lakini nilivyokumbuka debate zake Makerere na Edinburgh, Fabian Society na alivyopenda kumsoma John Stuart Mill nikasema si ajabu.
Tatizo huyu wa sasa sijui hata kama John Stuart Mill kashawahi kumsikia au anaelewa Fabian Society inasimamia nini.
Hiyo ya FB ni video?