Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Nimesikia baadhi ya watu wakipendekeza Uraisi uweze kupingwa Mahakamani akiwemo Mzee Shivji, binafsi napinga hilo na kwamba ibakie kama ilivyo sasa hivi kwamba Raisi wa JMTZ akishatangazwa ndiye Raisi na kila kitu kiishie hapo!
Na sababu ya kusema hivi ni ndogo tu, leo hii TanZania tukianza mambo ya kupinga Uraisi Mahakamani basi tutakaa miaka hata mitano bila ya kuwa na Raisi mpya kwani kila mtu ataenda kufungua kesi Mahakamni kupinga kama vile ilivyo kwenye Ubunge na hili litatuchelewesha tu kwenye mambo ya kimaendeleo, nchi yetu bado haijafikia huko, kwa sasa hivii anayeshinda na atakayetangazwa na Tume ndiye Raisi wa JMTZ na ibakie hivyo!
Kinyume na hapo ni chaos tu, sisi Waafrika bado hatujaweza kufikia huko, kuna sababu kwa nini waliweka huwo utaratibu, kwa maana wanajua fika kwamba Mwafrika hakubali kushindwa hata siku moja, mfano mdogo mpaka leo hii fisadi Lowasa hajawahi kutamka wazi kwamba kashindwa uchaguzi kwanza alikataa wakati Dunia nzima inafahamu na inatambua kwamba alishindwa tena kwa tofauti kubwa sana, sasa kungekuwa na kwenda Mahakamani ina maana mpaka leo hii bado Kikwete angekuwa Raisi, na mambo kama Elimu bure kwa wote yangesubiri, ukusanyaji wa trilioni 1.3 kodi ungesubiri, marufuku ya safari za nje na semina zisizokuwa na tija pia zingesubiri mpaka mshindi apatikane na angepatikana vipi? Kwa maana ambaye angetangazwa mshindi angekata rufaa na mwishowe kuwa total chaos!
Hivyo napinga Uraisi kupingwa Mahakamani kwani kuna sababu kwa nini waliweka hivyo!