Napendekeza namba moja ya wakala kwa mitandao yote ya simu

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,063
40,724
Yaani badala ya wakala kubandika namba za kutolea pesa za mitandao tofauti tofauti, aweke namba moja tu ya wakala na wateja wenye line za mitandao yote waweze kutoa pesa kwa kutumia namba hiyo hiyo moja, halafu wenye mitandao watagawana wenyewe pesa huko kwa kutumia automatic system watakayojiwekea.

Inakera sana unataka kutoa pesa Tigo halafu wakala anakwambia labda utoa Voda, Tigo sina float. Au unataka kuwe pesa Airtel halafu wakala anakwambia labda weka Tigo, Airtel sina float, inakera sana.

Ni kama mabenki yalivyofanya kwa kutumia ATM za UMOJA ambapo mteja wa benki yeyote ile iliyounganishwa na UMOJA ATMs anaweza kwenda kutoa pesa kwenye ATM hizo halafu wao wanapigiana hesabu wao kwa wao automatically na kusettle accounts, hii imesaidia sana maana ingebidi kila benki iweke ATM yake kila kona ya nchi kitu ambacho kingekuwa ni ghali sana.

Hivi nimeeleweka kweli?
================================
Update: 19/06/2020
B28DEDF8-97A3-48ED-BA58-38008FF50D62.jpeg

==========================
Update: 26/10/2022
Tigo na Zantel wameanza kutumia namba moja ya uwakala, mitandao mingine ya simu kujiunga hivi punde.
 
Faida nyingine ninayo ona ni kwamba hata mtu ambae hana mawakala wengi kwa sasa, mfano TTCL, automatically na yeye anakuwa na mawakala nchi nzima, just like that...! Kwakuwa TTCL ni ya serikali, basi serikali iweke msukumo kwenye hili ili walau kuipa TTCL a fighting chance!
 
Na nyie mliochelewa kuingia darasani kaeni hilo benchi la mbele kabisa niwaone vizuri...
 
Faida nyingine ninayo ona ni kwamba hata mtu ambae hana mawakala wengi kwa sasa, mfano TTCL, automatically na yeye anakuwa na mawakala nchi nzima, just like that...! Kwakuwa TTCL ni ya serikali, basi serikali iweke msukumo kwenye hili ili walau kuipa TTCL a fighting chance!
wengine watumie brains na resources ku-innovate halafu wazembe wazembe wasiojua hata maana ya customer care wapate mteremko? Acha mizaha Mkuu.
 
... wengine watumie brains na resources ku-innovate halafu wazembe wazembe wasiojua hata maana ya customer care wapate mteremko? Acha mizaha Mkuu.
Ofcourse kutakuwa na gharama ya kuingia kwenye huo mfumo, mfano UMOJA ATM's kila newcomer lazima alipe entry fee ili kuweza kuingizwa kwenye mfumo, na ni pesa nyingi unalipa, hivyo hakuna mteremko. Besides, haya makampuni binafsi yameshavuna vya kutosha, ni wakati sasa wagive back kwa serikali kupitia TTCL, kwani TCRA ikatunga muswada na bunge/JPM akaupitisha kuwa sheria, nani wa kubisha? Hutaki ondoka...
 
... yaani serikali itunge sheria kulazimisha makampuni binafsi kuungana ili kuwabeba wazembe? Labda Tanzania pekee!
 
... yaani serikali itunge sheria kulazimisha makampuni binafsi kuungana ili kuwabeba wazembe? Labda Tanzania pekee!
Mbona ilitungwa sheria ya kuwalazimisha kuuza hisa, bunge ni bunge na sheria ni sheria.
 
Idea poa sana.

Sasa sijajua kampuni gani itakuwa inamiliki hiyo namba moja.
Inamilikiwa na trustee ya hizo kampuni zote za simu, na panaweza pakafungulia escrow account mahali just in case pakatokea utata
 
Mawazo yako ni constructive. Yapo kumsaidia sana sana mtumiaji (sisi wananchi).

Tatizo hao wenye mitandao wapo ili watusaidie sisi au watunyonye?
 
Back
Top Bottom