Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,650
- 119,257
Wanabodi,
Nimeangalia kipindi cha Maswali ya Moja kwa Moja kwa Waziri Mkuu.
Nimeshuhudia Waziri Mkuu akiulizwa maswali ya msingi kabisa, lakini kabla Waziri Mkuu hajajibu, Naibu Spika alikuwa akimjibia.
Hii inaonyesha uwezo mdogo wa Naibu Spika kuchanganua kati ya maswali ya kisheria, kikatiba na kisera, hoja pekee ambazo Waziri Mkuu hakupaswa kuzijibu, ni hoja za kesi zilizoko mahakamani. Lakini swali la Mhe.Mbowe lilikuwa very valid.
Hivyo nashauri kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu, Waziri Mkuu aachwe ili ajibu maswali ya Wabunge, na ikionekana Mhe. Spika au Naibu Spika nao wana hamu ya kuulizwa maswali ya papo kwa papo, Bunge liandae kanuni, ili pia kiwepo kipindi cha maswali kwa Spika.
Ni pendekezo tuu, mnalionaje? .
Paskali