sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,682
- 1,110
Maneno na kauli tutoazo zinaishi ndani ya akili zetu, ni vigumu kufuta kitu kilicho jengwa akilini ndo maana tukasema, tuweke akiba ya maneno ili baadae tuweze kujua nini cha kuzungumzia.
SOMA: Mawaziri mizigo waibuliwa tena! Yupo Chiza wa Kilimo
Mh Nape Nnauye akiwa katibu mwenezi alifanya kazi kubwa sana ya kykipigania chama katika harakati za kurudisha imani ya wananchi, pamoja na kutatua kero za wananchi.
Akiwa na katibu mkuu mh. Abraham Kinana waliwaibua mawaziri mizigo, katika serikali ya awamu ya nne, miongoni mwao alikuwepo mh. Christopher Chizza, aliyekuwa waziri wa kilimo.
Katika hoja zake alikemea utendaji mbovu wa mh. Huyo na kumuita waziri mzigo miongoni mwa wenzake watano. Wana wa Buyugu waliliona hilo, kupitia mchakato wa uchaguzi alidondokea pua.
Mh Nape, yule yule aliyemuona akiwa mtendaji wa chama na chama ndicho kilichoisimamia serikali yake yupo Jimboni Buyugu kule kule alipomtambulisha kama waziri mzigo, ana mnadi mzigo kuwa Mbunge ili aendelee kuwa mzigo kwa wapiga kura. Hii imekaaje, kwanini tunashindwa kuishi kwenye kile tulicho kiamini kuliko kuonekana vuvuzela (mpiga kelele)!!!!
Iko hivi, kwa kutokutambua umuhimu wa watu muhimu jimboni Buyugu CCM kwa makusudi bila hata kuwashirikisha wananchi kuwa mzigo-mtu yule ameshatuliwa ule mzigo na sasa ana stahili kuwaongoza wana wa Buyugu.
Nimtake mh. Nape awe mwepesi wa kuhifadhi kumbukumbu ili kuweka mambo sahihi kuliko kusimamia asicho kiamini kwa kuwa wanatafuta kuongeza column ndani ya bunge.
Buyungu haihitaji Mbunge mzigo, inataka viongozi moto wenye kuweza kupambana na changamoto ndani ya jimbo kwa kipo mustakabali wa maendeleo ya Buyugu. Haiwezekani waziri mzigo asiwe Mbunge mzigo, wana Buyugu msijubali kuuziwa kipande cha chupa kwa thamani lulu, watch out, time will tell.