Nape: Wanachama wengi CCM mamluki; Asema asilimia 80 ya Wananchi ni Wanachama Wa CCM

Nnauye ameongeza kuwa ndani ya sekretarieti yao wamekubaliana kuunda tume ya kumtafuta mgombea bora wa kiti cha Urais ambaye anakubalika ndani ya chama na jamii.

Hilo ni kaburi la CCM ... come 2015, lazima CCM igawanyike na hasa kama makundi yaliyo ndani ya chama hayatavunjwa.

Niliposoma summary ya Report ya Task Force, walipendekeza kwamba wabadilishe utaratibu wa kupata mgombea urais. Kama utaratibu wa kutumia TUME ndo utaratibu mpya, kwa maoni yangu sioni kama wanaboresha bali wanazidi kuharibu zaidi.

Je, TUME itajuaje kwamba mgombea fulani anakubalika zaidi kuliko wagombea wengine? Haya ndio yale mambo ya kura za maoni kukata majina ya baadhi ya wagombea kwa sababu nyepesi za rushwa, uchanga kisiasa, uraia na mengineyo. Kutumia TUME kuna-promote nepotism, haina tofauti na Rais anayemaliza muda wake ku-pick candidate kwa kutumia kivuli cha tume.

Ninasubiri kwa shauku kubwa kuona hayo mabadiliko ya utaratibu wa kumpata mgombea urais kupitia CCM na pia mabadiliko ya uchaguzi wa wajumbe wa NEC kupitia kwenye wilaya zao.
 
08_10_hxqb4f.jpg Young Brigadier Gamba Boy
 
Back
Top Bottom