Nape uko wapi TBC inadhalilika

Nyakarungu

JF-Expert Member
May 1, 2011
472
377
Siko na furaha ninapoona Rais anatumia clouds tv, kutangaza mshahara, anapiga simu kupongeza watangazaji na kueleza wazi kwamba yeye ni mtazamaji namba moja wao.

Ninazidi kushangaa napomuona Mkuu wa mkoa akiitumia clouds kama media yake halisi namba moja kuhudhuria vipindi mbalimbali akizidi kuipaisha na kuidhalilisha tbc

Sababu kubwa ya Hawa viongozi kuitumia clouds hivyo au kuwa watazamaji na kuonyesha mahaba yote hayo hadharani ni kwa sababu wanaamini clouds inatazamwa na watu wengi kwa sababu ya ubunifu wa watangazaji wake na utawala wake

Lakini tukumbuke kupendeza kwa vipindi na vipindi sio jambo la miujiza bali ni kwa sababu za kiutawala kuwa wabunifu na watangazaji kuwa na vipaji vya kucheza na audience na sio suala la miujiza haliji automatical kabisa,

Mh, Waziri wa habari naomba uchokonoe TBC na utawala wao ili wafahamu namna ya kwenda na wakati na namna ya kuvaa uhitaji wa watazamaji kama inavyotakiwa na ulimwengu wa kijiditali

Vyeti tu havisaidii sana ikiwa bado watangazaji hawana extra creativity na management haina utayari wa kupokea mawazo ya watangazaji

Mh, Waziri chokonoa huko TBC wape ushauri na kuwaelekeza hata kuiga na kuboresha mazuri ya wengine ili TBC iwe na mvuto, ili sasa hata Rais akitaka kutuma salaam kwa watu wa kijiji chochote hata za utani aitumie TBC na sio private media, kwa sababu hii inasababisha tbc ionekane haina umuhimu

Siku ile amewapigia clouds tulijua anataka kutoa sreet cover ili siku hiyo watu wasahau mbwembwe za UKAWA, lakini pia siku ya wajinga akatuma ujumbe clouds na watu tukadhani kwa kuwa ni siku ya wajinga ameamua kutumia clouds tu ingawa alituma ujumbe wa kweli lakini kwenye siku ya wajinga kwenda clouds, hivyo wengine hatukupata shida sana

Lakini namuona mkuu wa mkoa wa dsm sio mara moja kila wakati anaonekana clouds akifafanua mambo kadhaa,

hii sio sawa kwa tbc
 
Huna kazi ya kufanya wewe. Inabidi upelekwe kambini ukalime...unataka kupambana na Rais Magufuli utaweza mziki wakeee
 
TBC inahitaji marekebisho makubwa sana ionekane ya kitaifa. Na ili iwe nzuri ipunguze ukada waje na vipindi bora enzi za Tindo mhando TBC ilikua vzuri sana
 
Back
Top Bottom