Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Mgombe Ubunge wa jimbo la Mtama kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Nape Moses Nnauye amewasisitiza wananchi wa jimbo la Kilwa Kaskazini kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura ili kumchagua mgombea Urais wa chama hicho Dkt. Samia Suluhu Hassan sambamba na Mbunge na Madiwani wake kutokana na kile alichoeleza kuwa mgombea huyo ndio 'Original' na kwamba wengine ni 'photocopy'
Ameeleza hayo Septemba 10.2025. Alipokuwa akizungumza na wananchi wa eneo hilo kama mgeni rasmi wa hafla ya uzinduzi wa kampeni za mgombea Ubunge wa jimbo hilo Kinjeketile Ngombale Mwiru, ambapo pia amesema, ambapo amesema Dkt. Samia katika kipindi chake kama Makamu wa Rais na baadaye kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametekeleza majukumu yake kikamilifu
"Sisi Chama cha Mapinduzi, tumemsimamisha Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuna vyama vingine vimesimamisha wagombea wao, mimi sina maneno nao kwa sababu wote wasindikizaji, yupo mmoja mwenye shughuli yake anaitwa Samia, na mtu mwenye akili timamu hawezi kuhangaika na photocopy wakati original ipo" -Nape
Ameongeza kuwa mataifa mengi hujikuta katika hali ya machafuko baada kujitokeza kwa mazingira kama yaliyotokea Tanzania mwaka 2021 (ya kufariki Rais aliyekuwa madarakani), lakini hapa Tanzania aliyekuwa Makamu wa Rais wakati huo Dkt. Samia Suluhu Hassan aliapishwa kuwa Rais na amenyesha utayari wa kuiongoza Tanzania licha ya kwamba awali hakujiandaa kushika nafasi hiyo
Aidha, Nape amesisitiza kuwa miradi yote ya maendeleo aliyoipokea Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoka kwa mtangulizi wake (Hayati Dkt. John Pombe Magufuli) imeendelea kiukamilifu zaidi ya ilivyokuwa awali
"Wakina mama wanaweza, na kama tulimjaribu miaka minne (4) hatuna sababu ya kumnyima miaka mingine mitano (5), amethibitisha anaweza" -Nape
Ameongeza kuwa licha ya msigano uliokuwepo kwenye siasa hapa nchini lakini Dkt. Samia Suluhu Hassan aliruhusu uhuru kwa wanasiana na mikutano ya hadhara kuendelea licha ya kushambuliwa kwa maneno
Aidha, ili kuchagiza maendeleo amesema kiongozi huyo alisisitiza ulipaji kodi wa haki hali iliyopelekea miradi ya maendeleo kukamilika.