Nape nimekuona, Nafurahi kuonesha wazi kuwa ndani ya chama kuna tatizo la kutosikiliza wananchi wanataka nini na hasa wakati wa chaguzi. Umeonesha wazi kuwa ulidhulumiwa nafasi ya kugombea ubunge UBUNGO. Lakini umekuwa mwepesi sana kusema kuwa Jimbo lilikuwa wazi kwa ajili yako. Umenishangaza sana uliposema kuwa ARUSHA ki kama kunywa maji kwenye glass hakuna upinzani unaoitisha CCM. Propaganda ni nzuri lakini vitani propaganda ni nzuri kuwaandaa wanajeshi katika hali ngumu kuliko uhalisia ili washinde kirahisi kuliko kuwadanganya wakakuta hali si nzuri kwa upande wao. Itachukua muda kuibadili system na vita hiyo siyo rahisi kama unavyo vikiri. Unaopingana nao ndani ya Chama wana wamewekeza katika sector na taasisi karibu zote ndani ya nchi, unapaswa kujua kuwa vita unayoizungumzia siyo yako na unaowaona, adui unayepigana nae haonekani jiandae kwa hali hiyo. Nakutakia kazi njema.