Jallen
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 517
- 196
Sina unasaba na chama hiki ila hawa watu ndio waliorudisha imani ya chama kwa watu. Hawa ndugu walizunguka Tanzania nzima wakihamisha wanachama na wananchi kuhusu CCM
Walipiga kelele kuhusu Waziri wa maji Maghembe waziri wa kilimo kuwa hawawajibiki ipasavyo kuhudumia wananchi.
Kazi aliyoifanyia chama na hata wakati wa kampeni ni kubwa sana. Sijui ni kwa nini mkuu ameamua hivyo tena hajaondolewa kwa uzembe bali kwa kusimamia haki.
Sasa ni nani atakayejitokeza mbele kupigania wanyonge, wanaoonewa, wanaodhulumiwa? Kama watetezi wao wanaondolewa? Hata kama yapo mapungufu yake lakini kwa jambo alilolisimamia alipaswa kupongezwa na kila mpenda haki.
Lakini naona kama Mungu anatupitisha huku kutukumbusha jambo fulani. Naona ukombozi wa tabaka la wanyonge ukitimia. Naona utawala ukifarakana, naona mwisho wa hiki chama ukijongea kwa kasi.
Ni wakati wetu kama taifa kupokea mabadiliko haya yanayokuja kwa kasi. Tudai kwa nguvu yale tuliyoayaacha kama katiba mpya. Huu ni mwanzo mwema kwa wapenda mageuzi.
Hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho, naam mwanzo wa mwisho huo umeanza.