Nape ngoja nikusaidie,,,, | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape ngoja nikusaidie,,,,

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CHEMPO, Jun 6, 2012.

 1. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Najua nafasi uliyonayo ni nafasi za watoto wa vigogo ila hilo tuachane nalo.
  Ndugu yangu nape kazi unayofanya kukiimarisha chama chako kwa mikutano na maandamano ni kazi bure. Nini serikali yako ya CCM ifanye ilikukiimarisha chama:-

  (1)kupambana na mfumuko wa bei ya vyakula na huduma za msingi zinazomgusa mwananchi moja kwa moja.

  (2)kuongeza pato la mtu mmoja mmoja, hii hasa kwa wafanyakazi,wapeni mishahara itakayowawezesha kuishi,tofauti na hapo hawa ndo watakaowamaliza 2015...mkilifanikisha hili nakuapia hamtapata upinzani wowote
   
 2. Ericus Kimasha

  Ericus Kimasha Verified User

  #2
  Jun 6, 2012
  Joined: Oct 27, 2006
  Messages: 488
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 60
  Counter attacks za CCM kwa CHADEMA zilipaswa zije na maudhui ya utofauti kati ya chama Tawala na Chama Kilicho nje ya Utawala. Badala ya kwenda kwa mkakati wa kushambulia majukwaani, CCM ingeshambulia kero na matatizo yanayoipa CHADEMA nguvu majukwaani na mitaani.

  CCM ingelipiza kwa kutafuta suluhisho na kuondoa matatizo yanayozidi kuwa sugu na ambayo kwa vyovyote yataleta madhara makubwa kwa jamii na Taifa siku si nyingi.

  Kwa mfano;


  1. CCM ingejidhatiti katika kubuni na kutekeleza mikakati inaokabiliana au kutoa suluhisho la changamoto ya ajira hasa kwa vijana (Nape Jr tuwasiliane kwenye hili).
  2. CCM ingehakikisha gharama za maisha hazipandi kupitia utekelezaji wa sera na maagizo ambayo imekuwa ikitoa

  Hivi vitu vikifanyika wala huitaji kwenda majukwaani ili uwafundishe watu uongo wa CHADEMA. Watanzania wa sasa wana macho yanayoona, masikio yanayosikia, akili zinazochambua mambo na utashi katika maamuzi. Suala la CCM nao kwenda na maneno matupu ilihali tayari wana dola, ni kumwongezea CHADEMA "Benefit of Doubt" kwamba labda huyu anaweza kufanya kweli akipewa dola.

  Wanachokisema CHADEMA si kigeni; CCM pia inakijua, Lowassa anakijua na Mh. Rais naye anakijua tena kwa ufasaha kupiti Ripoti Maalumu ya Uchumi aliyopewa mwaka 2007.

  Bora serikali ya ccm ikaonekana inasaidiwa/inaamshwa na wapinzani kufikiri/kutenda kuliko kukataa mapendekezo yao, huku isifanye lolote kubadili hali mbaya kwenye jamii. Yale yanayotekelezeka na kuleta ustawi kwa Watanzania yapokelewe. Mfano, Mkapa alikubali kuondoa kodi ya kichwa (hii ilikuwa sera ya CUF) lakini ilileta unafuu na kuwanufaisha Watanzania wote.

  Iwapo ccm watakuwa wakifanyia kazi kwa vitendo, haraka na ufasaha mambo ya msingi yanayoipaisha CHADEMA, nguvu ya CHADEMA na mvuto kwa wananchi unaweza kukabilika. Maana kwa mbinu hii CHADEMA watabaki kuonekana kama Wanadharia na CCM kama Watendaji.

  Tunajenga nchi moja.
   
 3. i

  iseesa JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Well said CHEMPO. Good advice to Nape kuliko kazi anayofanya sasa ya kujaribu 'kuupaka upepo rangi' au kujaza upepo kwenye gunia la katani
   
 4. K

  KIMBULU Member

  #4
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nape na wenzake wanajua yote hayo ILA Upeo wao wa kuyashughulikia na serikali yao ndo umefikia hapo.

  Kama unategemea mengine utasubiri saana tu.

  JAMANI yale yanayohitaji rasilimali fedha, serikali haina.

  Mfumo wa bei kwa mfano kuutatua to some extent unahitaji subsidy kwa Importers wa mafuta, fedha ambayo haipo.
   
 5. t

  tabu kuishi JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 354
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wachumia tumbo hao na ccm yao ya kubumba
   
 6. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Sikio la kufa ...............
   
 7. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ccm ishakuwa siku ya kufa nyani.................................
   
 8. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
   
 9. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wakubwa! Unapoambiwa "sikio la kufa halisikii dawa" ina maanisha haswa halisikii dawa,......hata CCM wangefanya mema makubwa kiasi gani kwa mtu kama mimi Ruhazwe JR hawanishawishi:,

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,497
  Likes Received: 19,909
  Trophy Points: 280
  anaenda kijijini kuwadanganya wazee na vibibi ambayo hawajui kitu akiwaambia inflation imeshuka sana wanapiga makofi hawajui hata ni nini wanafikiri labda ni mafuta ya taa.

  wao wanaangalia zile kanga na kofia na tisheti wanazopewa na Nape mengine hawana time nayo ,..hawa ndio watu anaowapenda Nape, si mmeona hapa tumembana anaanza kusema oo njooni na Majina yenu halisi mara aoo mwanaume unajificha nyuma ya ID sasa hizi nazo hoja?

  ccm wanapenda sana kulipa visasi anataka uje na ID yako ili akujue akulishe sumu kama walivyomlisha mwakyembe .
  ccm walivyo na roho mbaya wanaweeza kunywa uji wa mgonjwa mahututi
   
 11. Ericus Kimasha

  Ericus Kimasha Verified User

  #11
  Jun 6, 2012
  Joined: Oct 27, 2006
  Messages: 488
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 60
  CHEMPO,
  Nimekurekebishia maana ulipangua html codes na kuvuluga maandishi ya jibu lako.
  Asante pia kwa kuanzisha mada
   
 12. m

  mwanawaadam New Member

  #12
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nape ni mnafiki sana na kama yeye nimkweli atwambie huyu Rz1 haya majengo anayoporomosha kwenye baadhi ya Mikoa
  pesa kapata wapi kwamda mfupi wa kipindi cha utawala huu? kisha atwambie pesa tunazodanganywa kuwa walirudisha ziko wapi mbona mpaka leo mchanganuo wake hatujui wala zimefaya nini hatujui.je itakuwa vibaya kama tukisema kuwa ndozinaporomosha hayo majengo tutakosea? nape jibu hoja
   
 13. k

  kaka dj Member

  #13
  Jun 6, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kwa jinsi ilivyozoeleka siku zote anaeyekimbizwa umsifu aneyemkimbiza kwani huwa anamuongezea ujasiri na hali zaidi ya kushindana na mpinzani wake, lakini kwa chama kilicho kaa madarakani kukimbilia majukwaani na maandamano ambazo ni "sera za wapinzani"(kwani ndio sehemu pekee za upinzani kujieleza) ili kuwakimbiza uko na wao kuwa walalamikaji zaidi ya watendaji ukizingatia kuwa wameshika DOLA sidhani kama itasaidia chochote wakati huu. waswaili usema maji yakisha mwagika hayazoleki.
   
 14. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #14
  Jun 6, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  pamoja
   
 15. M

  Makyomwango JF-Expert Member

  #15
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 323
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Siyo kweli kwambe upeo wa Nape na magamba umefikia mwisho ila wako kimaslahi zaidi. Nape na wenzake ni wako katika kundi la wanafiki, wasio wazalendo na na wabinafsi kupita kiasi. Ni watu wanaofurahia na kuushangilia umasikini wa watanganyika walio wengi. Kupata kwao kwatosha wengine watajijua wenyewe. Hawajali kabisa hali za maisha duni za baba zao, mama zao, kaka zao, binamu zao na hata rafiki zao. Wajali kwa lipi ilihali wao wamepata!
   
 16. d

  dguyana JF-Expert Member

  #16
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu Nape mngemwacha tu wala si wa kujadili. Nadhan anajua ukweli lakini atafanyaje tena wakati yeye ndio anawatumikia waliompa kazi. Kama ni wewe je ungefanyaje?? Mwacheni tu anaujua ukweli ila yupo kazini mwenzetu.
   
 17. Suzie

  Suzie JF-Expert Member

  #17
  Jun 6, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 1,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Khaaaaa eti inflation imeshuka wanajua mafuta taa umeniacha hoi
   
 18. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #18
  Jun 6, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,157
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  ni heri uende mochwari ukaelimishe maiti kuliko kupoteza mda wako kumuelimisha mtu kama Nape
   
 19. Medical Dictionary

  Medical Dictionary JF-Expert Member

  #19
  Jun 6, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 1,053
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  too late..
   
 20. Tangopori

  Tangopori JF-Expert Member

  #20
  Jun 6, 2012
  Joined: May 11, 2012
  Messages: 1,614
  Likes Received: 274
  Trophy Points: 180
  niambie dogo nasikia leo mmetia timu hapa skul
   
Loading...