Chikumba one
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 1,012
- 1,647
Mara nyingi Katibu Mwenezi wa CCM amenukuliwa akisema Mheshimiwa Warioba na Wazee wenye umri kama wake ni watu wanaosubiri "kufa". Naamini alikusudia kututaka Watanzania tumpuuzie Jaji Warioba na Wazee wenye msimamo kama wake hasa waliopo kwenye tume ya Rais iliyokusanya maoni juu ya Katiba mpya. Kwa chama makini na hasa kinachoongoza dola, kauli hii ilitosha kumvua wadhifa wake na pengine kumfuta uanachama kwa kuwazalilisha Wazee wetu ambao wamepoteza nguvu zao nyingi kukijenga chama ambacho leo ndio kinachompa kula Nape na familia yake! Ajabu mtu huyu bado anaendelea na wadhifa wake, na si ajabu wapo waliompongeza kwa kauli yake yenye upofu wa hekima!
Nape anasahau kwamba Wazee ni hazina adimu sana na muhimu kwa maisha ya binadamu yeyote hasa kwa vijana kama yeye. Kwa kuzingatia UKWELI huo, leo CCM ina kamati ya Ushauri inayoundwa na Wazee kama wanaopuuzwa na kijana Nape. Mara nyingi Mheshimiwa Rais amekuwa na kawaida ya kuzungumza na Wazee wa Dar es salaam lakini akiwa na lengo la kufikisha ujumbe wake kwa Watanzania wote popote tulipo. Swali langu ni Je, Nape huwa anajisikiaje katika nafsi yake? Je, si kweli kwamba huwa anamshangaa Mheshimiwa Rais wetu kwa kuzungumza na Wazee wanaosubiri kufa ambao wengi wao ni wanachama wa CCM?
Najua kuna busara na hekima ya kutosha hutumika kupendekeza kundi la wazee kuwa kundi wakilishi kwa Rais anapotaka kuzungumza na Wananchi, ni utaratibu ambao hata Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alikuwa akiutumia! Je tuamini kwamba vijana tukipata madaraka na uongozi huwa tunachanganyikiwa na kuwapuuza wazee wetu ambao wametuamini kwa nia njema kabisa kwa kutupa nafasi hizi tulizonazo sasa? Hata kama rekodi inaonyesha vijana wengi hupewa madaraka na uongozi kwa upendeleo zaidi kuliko uwezo wa kijana husika, bado haiwezi kuwa kigezo cha kuishiwa nidhamu kiasi cha kuwatusi wazee wetu. Tayari Kijana Makonda nae kaanza kupitia njia ya Nape.
Je kuna mabadiliko katika mtaala wa kuwaandaa vijana ndani ya Chama? Kama sio, mbona vijana wa zamani hawakuwa hivi? Bado sielewi kwa nini Nape anaendelea kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi ndani ya Chama, wadhifa ambao ndio Kauli na matamko mengi ya Chama hupitia! Kama hili halijaonekana kuwa ni tatizo, basi kuna tatizo ndani ya Chama!
Leo Kauli na matamko mengi yatolewayo na chama yamekuwa yakipuuzwa na kuchukuliwa kwa uzito usiostahili kwa kuwa tu yanatoka kupitia kinywa cha Nape! Watu wengi wenye busara wamempuuzia kijana huyu kiasi kwamba hakuna anaemjali! Kwa sasa kauli za Wasemaji wa vyama vya upinzani zina mvuto kuliko za chama tawala! Hili halikubaliki hata kidogo! Wazee na watu wenye busara ndani ya chama wamejitenga na kukaa kimya wakiwaachia vijana hawa kukivuruga chama! Huwezi kujenga chama kwa kuwatukana Waasisi wa chama na viongozi wa vyama vya upinzani!
Chama hujengwa kwa hoja zenye ushawishi ndani ya jamii, hakuna aliezaliwa akiwa mwanachama wa chama cha siasa, bali wanachama hupatikana kwa kuvutiwa na sera, hoja na ushawishi kutoka kwa viongozi wa vyama wenye uwezo na weredi! Idara ya Itikadi na Uenezi ndiyo wenye jukumu hili kwa chama chochote cha siasa! Haipo na haiwezi kuwa hivyo kupitia kwa Nape Moses Nnauye wa CCM! Mpaka sasa hakuna alieliona hili!
Tathmini inaonyesha upinzani unazidi kukua na kukinyima usingizi Chama tawala! Wakati Vijana ni chachu ya Maendeleo, Wazee ni hazina iliyojaa hekima, busara na uzoefu mwingi katika kuyafikia maendeleo, kamwe hawawezi kuwa watu wanaosubiri kufa! kifo ni pitio kwa kila kiumbe, haijalishi umri ulionao! Ni wakati wa Nape kujitathmini!