Nape na waalimu Mafinga

Gizakuu

Member
Apr 29, 2012
38
13
Nashauri si busara kabisa kubeza hizi juhudi za magamba za kurudisha imani ya watu mbalimbali nchini kwao. Leo Mafinga Nape amekutana na waalimu zaidi ya 360 na amekuwa na amzungumzo nao kwa muda mrefu sanaaa! Juhudi hizi zitaturudisha nyuma sana kwenye ukombozi wa nchi tuwe macho na huyu.dogo!
 

Attachments

  • 1.jpg
    1.jpg
    144.1 KB · Views: 149
Wamekuja kwa hiari yao au wamelazimishwa na mwajiri wao kuja kuongea naye? Nadhani ni kinyume cha taratibu za ajira kwa mwajiri kutumia uwezo wake kushinikiza waajiriwa wake kwenda kusikiliza au kuongea na wanasiasa au viongozi wa chama fulani cha siasa. Hata kama yeye Nape ndo anawalipa posho na pesa ya kujikimu, bado siyo sahihi kwa mwajiri wao kutumiwa na wanasiasa.
 
Niliwaulimuuliza mmoja wa waalimu kama wameshinikizwa kuhudhuria mazungumzo hayo, akaanza kwa kunishangaa...." hivi mtu mzima anaweza lazimishwa kuja hapa?!! Sisi watu wazima TUMEOMBA WENYEWE KUKUTANA NA MWENYE SERIKALI AMBAYE NI CHAMA TAWALA, TUMWELEZE YANAYOTUKERA... hakuna aliyelazimishwa"
 
Tatizo asilimia kubwa ya walimu bongo ni valaza. Kama unamchukua mtu aliyeshindwa kufaulu mtihani then ndio akawe mwalimu unategemea nini hapo. Walimu makini wanaojua haki zao ni wale wenye degree, but hao wa chini yaani certificates na diploma, ni vilaza sana wengi wao na ndiyo wanaotuangusha. We kama huamini oa mwalimu then utathibitisha haya nisemayo.
 
mimi ni mwalimu najaribu kufikiria sababu ya hao walimu kukusanyika hapo nakosa sioni sana naona jinsi hao walimu walivyokosa uelewa wa mambo.haiwezekani lipo tatizo kwenye uelewa wa walimu hao.kwa sababu walimu wenye akili tulisha ona nini cha kuwafundisha watoto na maendeleo sio mabaya saana. Kama serikali haisikilisi tunajua cha kufanya .sasa hao walimu wa mafinga wanaishi tanzania gani, napata mashaka na uelewa wao.
 
Watanzania sio wa hivyo,wameshajua hiyo ni janja ya nyani,hata wafanye nini bado tutapambana nao tu.
Changes 4 new generation
 
tulisha sema hatuna haja ya kura za waalimu...

leo mmewakumbuka sio??

ila kwa sababu ya vinjaanjaa vyao watawasamehe bbwana..si unajua tena ualimu ni wto na sio ajiraa
 
Hao waalimu wajinga-wajinga wafukuzwe mara moja.Nasema ni wajinga kwa sababu naamini katika mkataba wao wa ajira hakuna sehemu pameainishwa kwamba Waalimu wakiwa na matatizo watakaa vikao na viongozi wa vyama vya siasa.Ina maana kwamba wizara ya elimu haina connection yoyote na watumishi wake? Au wizara inamtumia NAPE kama communication tool then,ina maana kwamba mwalimu asipokuwa na mahusiano ya karibu na ccm matatizo yake hayatashughulikiwa. Siasa na utumishi ni lazima vitenganishwe.Tatizo ninaloliona ni namna baadhi ya masomo yanayotolewa ni yale yanayomuandaa mtu kuwa zezeta,mwoga na anaeshindwa kujua network ya kutatua matatizo.Kwa vitendo hivyo vya waalimu wasiojitambua je,tutegemee idadi ya wanafunzi wenye kusimamia mambo kutokea? Siku ya mei mosi,1996:mwalimu Nyerere aliwakumbusha wakulima na wafanyakazi kazi kwamba BABA YAO NI UMOJA.
 
Hao walimu wanakutana na Nape Kama nani??
Naamini maneno ya wachangiaji hapo juu kua ni vilaza wa kutupwa!!
 
Haya ndiyo matokeo ya "UALIMU PASIPO ELIMU". Sasa kutoka kwa mbumbumbu kama hawa utegemee elimu gani.
 
Walimu wamejidhalilisha pamoja na DED,DEO na viongozi wa Halmshauri yao.Hivi kama hapo Walimu wakitoa malalamiko na maazimio nani anatekeleza wakati NEPI ni third party.Wote naamini ni vilaza siyo NEPI na walimu na viongozi wao wa Halmashauri.Ujinga kama wao huo hawezi kuondoa taifa ili katka utapiamlo wa maendeleo.
 
Niliwaulimuuliza mmoja wa waalimu kama wameshinikizwa kuhudhuria mazungumzo hayo, akaanza kwa kunishangaa...." hivi mtu mzima anaweza lazimishwa kuja hapa?!! Sisi watu wazima TUMEOMBA WENYEWE KUKUTANA NA MWENYE SERIKALI AMBAYE NI CHAMA TAWALA, TUMWELEZE YANAYOTUKERA... hakuna aliyelazimishwa"
Umejiuliza na kujijibu mwenyewe gamba
 
Kwa mwendo huu matatizo ya walimu hayatapata suluhisho, ktk hili nape ni nani? Masikini walimu! Ok wameongea na huyo kilaza leo, kesho watahitwa na mkama wataenda, kesho kutwa watahitwa na wasira na wengineo maana orodha ni ndefu, mwisho wa siku matatizo ni pale pale! Ninacho kiona hapo hawajajua mkombozi wao ni nani.
 
Nashauri si busara kabisa kubeza hizi juhudi za magamba za kurudisha imani ya watu mbalimbali nchini kwao. Leo Mafinga Nape amekutana na waalimu zaidi ya 360 na amekuwa na amzungumzo nao kwa muda mrefu sanaaa! Juhudi hizi zitaturudisha nyuma sana kwenye ukombozi wa nchi tuwe macho na huyu.dogo!

kukutana na walimu ni kitu kingine na kumuelewa ni kitu kingine.arumeru walikutana makundi mbalimbali ikiwemo walimu kila moja kwa wakati wake lakini siku ya mwisho walitoa hukumu,wenyewe mnaijua!
 
Labda Nape kaoa mwalimu, sasa hapo alikuwa anaongea na shemeji zake. otherwise no logic......!!!!!!!!!!!!!!!
 
Itakuwa anaongea nao kuhusu umuhimu wa sensa, kwani kuna mtu hapo!? Nape na hao walimu ni sawa na mbwa kala mbwa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom