Nape na katiba mpya vs Mimi na katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape na katiba mpya vs Mimi na katiba mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mito, May 17, 2012.

 1. mito

  mito JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,638
  Likes Received: 2,024
  Trophy Points: 280
  MGOMBEA BINAFSI KUWA PIGO KWA VYAMA VYA UPINZANI?

  Chama Cha Mapinduzi kama mdau miongoni mwa wenye haki kisheria kutoa maoni kuhusu mabadiliko ya Katiba, leo kimetangaza msimamo wake kuhusu mambo ambayo kinaona kwamba yanafaa kuwemo kwenye mdajala wa katiba mpya. Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dar es Salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (CCM), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema mapendekezo ya CCM yapo katika sehemu mbili. Nape alisema moja ya mambo ambayo haihofii kujadiliwa ni uwepo wa mgombea binafsi, akisema ikiwa ikiwa hilo litapita katika katiba mpya, itakauwa pigo zaidi kwa wapinzani kuliko CCM.“Sisi CCM hatuhofii hili la mgombea binafsi, kwanza likikubalika wapinzani ndio watakaoumia.. Unadhani kama kungekuwa na mgombea binafsi nani angehamia upinzani?” Nape alisema na kuhoji.

  Ifuatayo ni Taarifa Kamili kuhusu **** hilo la CCM hii hapa.


  Kwakuwa sheria inayosimamia mchakato wa mabadiliko ya Katiba nchini imevipa uhuru vyama vya siasa kushiriki kwenye mchakato wa Mabadiliko hayo ya Katiba. Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Dk Jakaya Mrisho Kikwete, Mei 13, 2012, walifanya semina kuhusu Mwongozo wa CCM katika kushiriki katika mjadala wa Katiba Mpya. Katika semina hiyo, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa walijadili maeneo ya Misingi Mikuu ya Taifa ambayo yanatakiwa kubaki ndani ya Katiba mpya; na Mambo ambayo hayagusi Misingi Mikuu ya Taifa lakini ni muhimu kwa nchi, mambo ambayo yako wazi kwa mjadala mpana. Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ilijadili na kukubaliana kuwa wanachama na wananchi kwa ujumla wahakikishe kuwa Misingi Mikuu ya Taifa letu inabaki katika Katiba Mpya itayoandikwa. Misingi mikuu iliyojadiliwa na kukubalika ibaki au iingie katika Katiba Mpya ni pamoja na:
  1. Kuwapo kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  2. Muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuwa wa Serikali mbili; Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  3. Kuendelea kuwapo kwa mihimili mitatu ya Dola (Serikali, Bunge na Mahakama).
  4. Kuendelea kuwapo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  5. Kuendelea kuwapo kwa Umoja wa Kitaifa, Amani, Utulivu, Usawa na Haki.
  6. Kufanyika kwa uchaguzi wa mara kwa mara katika vipindi maalumu na kuzingatia haki ya kupiga kura kwa kila mtu mwenye sifa zinazohitajika kwa mujibu wa sheria.
  7. Kuendeleza uhifadhi na ukuzaji wa Haki za Binadamu na kuheshimu usawa mbele ya sheria.
  8. Kuendeleza sera ya dola kutokuwa na dini rasmi, bali inaruhusu kila mtu awe na uhuru wa kufuata dini anayoitaka mwenyewe.
  9. Kuendeleza sera ya serikali kuwa ndiye mmiliki wa raslimali kuu za nchi, hususan Ardhi.
  10. Kuendeleza sera ya kuwapo kwa usimamizi madhubuti wa maadili ya viongozi. Kwa kuupa nguvu za kikatiba.
  11. Kuimarisha madaraka ya umma.
  12. Kuhamasisha Sera ya msingi ya kujitegemea.
  13. Kusimamia Usawa wa jinsia na haki za wanawake, watoto na makundi mengine maalumu katika jamii.
  14. Kusimamia Hifadhi ya mazingira.
  15. Na kuendelea kuwapo kwa Rais mtendaji.

  Mambo mengine mengine yaliyobaki, ambayo yanahusu masuala ya uendeshaji wa serikali, wananchi wapewe fursa ya kuchangia maoni yao kwa kadri kila mmoja anavyoona inafaa kwa kuzingatia maslahi ya Taifa letu. Mambo ambayo yapo wazi kwa mjadala mpana ni pamoja na haya yafuatayo;-
  1. Mambo yanayosababisha kuwapo kwa kero za Muungano zilizopo hususani Orodha ya mambo ya Muungano.
  2. Utaratibu wa uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
  3. Madaraka ya Rais.
  4. Taratibu za uteuzi wa Mawaziri/ Waziri mkuu.
  5. Utaratibu wa Uteuzi wa Tume huru ya uchaguzi.
  6. Swala la mgombea binafsi katika uchaguzi wa dola.
  7. Kuhusu muundo wa bunge/ baraza la wawakilishi na aina ya wabunge/ wawakilishi.
  8. Kuhoji mahakamani matokeo ya Uchaguzi wa Rais.
  9. Uwepo wa baraza la pili la kutunga sheria.
  10. Ukomo wa Idadi ya Wabunge.
  11. Mfumo wa mahakama.
  12. Nafasi ya Rais wa Zanzibar katika Uongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

  NAPE NNAUYE
  Katibu wa NEC
  Itikadi na Uenezi.

  Sasa ongeza haya ktk orodha ya Nape (ni mtizamo wangu lakini):

  1. Nadhani hakuna ubishi kuwa ktk katiba mpya wengi wetu tunataka zile presidential posts zipunguzwe kabisa kama siyo kuziondoa kabisa. Hii itasaidia kupata competent people na kuongeza uwajibikaji
  2. Pia mawaziri wasiwe wabunge, nadhani hili lilishaongelewa sana tu
  3. Wakuu wa Mikoa na Wilaya waondolewe kabisa, ni mzigo tu kwa serikali
  4. Mbunge/diwani akipoteza sifa za kuwawakilisha wananchi (e.g. kufuatia kifo, kujiuzuru, kutenguliwa na mahakama n.k) hakuna kurudiwa uchaguzi kwani ni kupoteza pesa za walipa kodi bure. Badala yake chama chake au chama kilichopata haki kiteue wa kushika nafasi hiyo. Kama hakuwa na chama basi wagombea binafsi wengine watagombea nafasi hiyo na wabunge watapiga kura kwa niaba ya wananchi.
  5. Kuwepo na ukomo wa umri wa kugombea nafasi za kisiasa hasa ubunge na udiwani ili kuwapa nafasi vijana na kuepuka influential people kung’ang’ania hizi nafasi, pia kuzuia wale wanaosinzia sinzia tu oyyo bungeni kwa sababu ya uzee
  6. Wabunge wa kuteuliwa na Rais (not more than ten members) wafutwe kabisa. Hii itaokoa pesa nyingi za walipa kodi, pia itaondoa mwanya wa kupeana ubunge kishkaji
  7. Nafasi za ubunge za upendeleo kwa wanawake (Special seats women members) nazo zifutwe. Hii nayo itaokoa pesa nyingi za walipa kodi, pia itaondoa mwanya wa kupeana kishkaji.
  8. Mtindo wa kupitisha maamuzi bungeni kwa njia ya kusema NDIO au HAPANA ufutwe kabisa. Badala yake ipigwe kura ya siri au uzito wa hoja na umuhimu wake kwa wananchi.
  9. Spika na naibu wake wasitoke miongoni mwa wabunge. Na wasitoke ktk chama cha siasa bali wawe wagombea binafsi, watapatikana kwa kupigiwa kura na wabunge
  10. Board members ktk taasisi mbalimbali za serikali wasiteuliwe kama ilivyo sasa ambapo wanapeana kishkaji tu. Wa-apply na wapatikane based on qualifications and their contributions to overall issues za taasisi husika
  Na wewe ongezea mengine basi, pia toa maoni yako kuhusu hayo hapo juu
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  ccm inawayumbisha, ilikuwa, na bado ina dola, ilishindwa nini kupeleka muswada mungeni ili kuyaingiza hayo mambo wanayoyapendekeza sasa!
  watueleze leo, mtikila alishinda kesi mahakamani dhidi ya serikali kuhusu mgombea binafsi, ccm ikishauriwa na chenge walipinga kwa kukata rufaa ambayo iliielekeza serikali kubadilisha sheria kupitia bunge, na hawajafanya hivyo mpaka sasa. Nani kawakurupusha!!!!!
  MAPENDEKEZO YA CCM YAPIGWE CHINI OUT RIGHT.
   
 3. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Mjadala wa katiba mpya ni wa wananchi wote siyo wa wanaCCM peke yao. CCM hawana haki au mamlaka yoyote ya kutuamlia nini kijadiliwe na nini kisijadiliwe. Tukikubali hilo tumeliwa. Hiyo Tume ikipita na kuanza kutuwekea mipaka ya kujadili tutajua inafanya kazi kwa maelekezo ya CCM. Tutaikataa. Hata kuvunja muungano ni moja ya hoja ambazo zitajadiliwa. Kama wengi wanataka muungano uvunjwe CCM wana haki gani ya kusema usivunjwe?
   
Loading...