Goliath mfalamagoha
JF-Expert Member
- Aug 3, 2012
- 602
- 2,505
Mheshimiwa Nape, nimekusikiliza jana, nimekuelewa sana..., unataka busara ipi hiyo itumike katika kuwashughulikia hawa "wanaodaiwa kuhusika na biashara haramu ya dawa za kulevya"!? Leo Nape unataka utaratibu wa kisheria uzingatiwe.., umesahau mengi kwa haraka sana..,
sawa.., sasa unataka busara ipi itumike kupambana na hawa wasanii 'walioko chini yako' (wewe ni waziri wa sanaa) wanaojihusisha na biashara hii haramu!? Wakati ule (wewe) na wenzako kule Dodoma mnaungana kutunyima sisi raia wa Kawaida haki yetu ya kuwatazama wabunge wetu (wawakilishi) haki ya kutazama bunge Mubashara, kwanini haukutumia busara hiyo kusililiza kelele za watanzania wale!? (uliongozwa na busara ipi kuweka bunge gizani, licha ya watanzania wengi kusema hapana!?)
Leo unapata wapi nguvu za kusema kwamba "Brand ya wasanii wale inachafuliwa"!? Kwanini usione kwamba "Brand ya bunge inakufa kwa kuliweka bunge gizani"!? Hebu bwana Nape, acha bwana Marconder aendelee na sanaa zake (apate kiki) wakati huo wewe ukifanikisha mpango wa kurejesha bunge "mubashara" kwa watanzania..,
Swali rahisi sana kwako wewe bwana Nape, "unaweza kukumbuka, ni lini wewe umewahi kutoa tuhuma kwa namna inayolinda brand za watu?" umesahau wakati ule unarekebu Lowassa, umesahau vita yako na Dr Slaa.., leo unataka "busara itumike"..,
zile porojo zenu za "watanzania wafanye kazi" mara "kurusha matangazo ni gharama" zimepitwa na wakati (waswahili wanaita, uongo na ulaghai laini), ukishindwa hili, basi acha (Marconder) awashughulikie hawa (casts) wake katika filamu yake hiyo.., hauna "usafi" huo wa kusema "haki ifuatwe" wakati wewe ulitunyima haki yetu ya msingi ya kupata habari bwana Nape!
Pia.., kama issue ni busara na kushauri mamlaka na watawala kufuata sheria na taratibu.., wewe Nape, ungeomba, Busara pia katika ukamataji wa Magurudumu ya pikipiki zipitazo katika barabara za mwendokasi.., au kwa sababu wameguswa marafiki zako, sasa unaanza kuumia.., wauza unga wapewe utetezi, wale Bodaboda nani mtetezi wao kule "sentro"!?
NB; ingawa mimi mwenyewe, kwenye (maigizo) yenu haya, sina imani na yoyote kati yenu (wewe au Marconder), naona sasa mmeanza kuingiliana kwenye mistari yenu, piga miluziiiiii.., "mbwa" apotee njia, matokeo kidato cha 4, pale MZIZIMA vipiiii?