nyumba kubwa
JF-Expert Member
- Oct 8, 2010
- 10,309
- 8,398
Namuunga mkono Nape, Lowasas hafai na hawezi kuwa Rais wa nchi ambayo ina wananchi wengi tu wasiopenda rushwa, hawa waliomo humu wanaomtetea Lowassa hawana uchungu na nchi yetu, ni wachumia tumbo na wabinafsi wamewaweka rehami mpaka watoto wao kwa ulafi wao, tusiwaruhusu watukatishe tamaa, haijalishi uropokaji wa Nape cha muhimu amekua consistent katika hilo, kama mafisadi hawakutoswa wakulaumiwa sio Nape ni unafiki na undumila kuwili wa mwenekiti wa chama chao, wote tunajua hatua ya kuwavua magamba mafisadi ni muhimu kwa muhtabali wa taifa letu, Nape did his job sasa angefanyaje wakti mwenyekiti wake hana uwezo wa kufanya maamuzi magumu na anajipendekeza kwa mafisadi? Big up Nape historia ndio itakayokuponya wakati hawa unaopambana nao hawaponi
Acha kupotosha watu weka chote nilichosema. Nilichosema ni kuwa yeyote anayekiuka taratibu za chama katika mchakato ANAJIONDELEA SIFA za kuwa mgombea wa chama hichi!(Labda Chama kiamue kutofuata taratibu zake chenyewe, na kikiziacha hakina namna ya kuendelea kuaminiwa)!
Sasa si swala la Lowassa ni swala la KILA ANAYEKIUKA TARATIBU!kama naye anakiuka anaingia kwenye mkumbo huo, sio kwasababu ni Lowassa ila kwasababu ni mwana CCM na taratibu za CCM haziruhusu! Sio swala la Nape ni swala la taratibu,kanuni na sheria zilizowekwa kabla hata Nape hajazaliwa!
Haiwezekani watu wagawe rushwa hovyo tukae kimya tu kisa anayegawa flani!!!! Hivi kuna uwezekano wa kuingia na kiti moto msikitini ukapigiwa makofi?!! Unaweza kupigiwa makofi na kupewa uongozi wa kanisa wakati humwamini Yesu Kristo?!! Watanzania tusiogope kusema ukweli maana ndio utakaoiponya nchi yetu.
Kama mnamgombea ana sifa atachaguliwa tu huna haja ya kuongezea sifa zake kwa rushwa! Haya si yangu ya CCM, na ni kwa madiwani, wabunge na hata urais!
HERI YA MWAKA MPYA 2014!
Mimi si CCM na wala sina mpango wa kuwa mmoja wao, lakini kwa kauli hii Nape amenikuna.
Kuchaguliwa Lowasa au fisadi mwingine anayefahamika kwa uhalifu huo itakuwa ni sawa na kuwakabidhi wapinzani Ikulu hata kabla ya uchaguzi.
CCM isijidanyanye; watanzania wa 2015 watakuwa tofauti kabisa na wale wa 2005 na wa 2010 walioichagua CCM kwa kuhongwa kofia, bangili, vikoi, sukari, kapelo na sifa za kijinga kijinga kama .... Ooh ana sura ya mvuto, handsome kana kwamba tulikuwa tunamchagulia Binti mchumba!
Chema chajiuza na kibaya chajitembeza; ndivyo alivyo fisadi papa huyu anayejipendekeza kwa watanzania, tena kwa kutumia fedha alizowaibia na anazoendelea kuwaibia kupitia Makampuni ya Symbion; Vodacom na ujambazi mwingine.
Mhalifu huyu anautafuta urais ili kuficha maovu yake na mashoga zake.
Acha kumpamba EL huyo ni FISADI NAMBA ONE.
Alijiuzuru kwa ajili ya ufiaadi wa RICHMOND
RICHARDWILIUM
Nape Sacha kumwandama Lowasa, haumwezi kwani anakubalika hataufanyeje. Lowassa ni mchapakazi na mwadilifu.