Watu
JF-Expert Member
- May 12, 2008
- 3,231
- 1,470
Maneno Kuntu haya
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa angebaki ndani ya chama hicho wangekuwa na mzigo mkubwa wa kuwaaminisha watu kuwa CCM si mafisadi.
Akizungumza katika mahojiano maalumu nyumbani kwake mjini Dodoma hivi karibuni Nnauye amesema: “Yeye alikuwa alama ya ufisadi alipoondoka aliturahisishia kazi. Watu walikuwa wanahusisha ufisadi na umaskini, walichoka na walikuwa radhi kuchagua hata jiwe lakini si CCM.”
“CCM ilifika pabaya, kelele zilizidi kwani tuhuma dhidi yake (Lowassa) zilikuwa zikikipaka matope chama. Wananchi walikuwa wameichoka Serikali yao kutokana na kuingia mikataba mibovu, rushwa, ufisadi na watu walikuwa wanafanya vitendo vya aibu na kujificha ndani ya chama.”