Nape aungwe mkono kukemea ufisadi-bawacha

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
Na George Boniphace

Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza (BAWACHA), Bi.Jane Kajoki , ameunga na kupongeza jitihada kubwa zinazofanywa hivi sasa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa CCM itikadi na Uenezi, Bw. Nape Nnauye, za kupinga na kukemea ufisadi ndani ya serikali na Chama chake.

Bi. Kajoki alitoa pongezi hizo juzi alipokuwa akizunumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake jijini hapa kuhusu hali ya kisiasa nchini na Mkoa wa Mwanza.

Alisema , Bw.Nnauye yuko sahihi kutoa mawazo yake hadharani kwa kuwakosoa wale wanaohujumu mali ya umma kwa kutumia nafasi walizonazo serikalini au ndani ya chama chake na kwamba wale wanaobeza juhudi hizo hawaitakii mema Tanzania hususani watu maskini.

Alisema wale wanao beza kiongozi huyo wa CCM hususani waliomo ndani ya chama chake wanaonekana kwamba wana lengo la kuficha madhambi yao ndani ya utumishi wao serikalini au vyama vyao.

Alisema Bw. Nnauye anatumia nafasi yake aliyonayo kisiasa kufikisha ujumbe kwa jamii ili nayo iwahukumu watu hao kupitia chaguzi zijazo kwa kuwanyima kura kutokana na madhambi yao waliyoyatenda hivyo anapaswa kuungwa mkono na si kubezwa.

Chanzo: Majira
 
Huyu mama naye yupo OP, hajui kuwa nape yupo kwenye mnyukano wa presidential election 2015 ndani ya chama chao cha magamba
 
Na George Boniphace
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza (BAWACHA), Bi.Jane Kajoki , ameunga na kupongeza jitihada kubwa zinazofanywa hivi sasa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa CCM itikadi na Uenezi, Bw. Nape Nnauye, za kupinga na kukemea ufisadi ndani ya serikali na Chama chake.
Bi. Kajoki alitoa pongezi hizo juzi alipokuwa akizunumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake jijini hapa kuhusu hali ya kisiasa nchini na Mkoa wa Mwanza.
Alisema , Bw.Nnauye yuko sahihi kutoa mawazo yake hadharani kwa kuwakosoa wale wanaohujumu mali ya umma kwa kutumia nafasi walizonazo serikalini au ndani ya chama chake na kwamba wale wanaobeza juhudi hizo hawaitakii mema Tanzania hususani watu maskini.
Alisema wale wanao beza kiongozi huyo wa CCM hususani waliomo ndani ya chama chake wanaonekana kwamba wana lengo la kuficha madhambi yao ndani ya utumishi wao serikalini au vyama vyao.
Alisema Bw. Nnauye anatumia nafasi yake aliyonayo kisiasa kufikisha ujumbe kwa jamii ili nayo iwahukumu watu hao kupitia chaguzi zijazo kwa kuwanyima kura kutokana na madhambi yao waliyoyatenda hivyo anapaswa kuungwa mkono na si kubezwa.

Chanzo: Majira
Kwani NAPE hajui kuwa JK ni gamba??????????
huyu mama inabidi achambue vizuri na sii jujuuu kama hii
 
Back
Top Bottom