Nape arushiwa kombora mkoani Ruvuma

Mar 23, 2012
64
13
Na Stephano Mango, Songea

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoani Ruvuma kimemtaka Katibu wahalmashauri kuu ya CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kuacha kuwadanganya wananchi kwa kuwapa matumaini ambayo yanaendelea kuwatesa kwa sababu ya kuokoachama ambacho kinaendelea kufa.

Wito huo umetolewa jana kwenye mikutano miwili tofauti yenye lengo la kuwahamasisha wananchi kuvua Gamba na kuvaa Gwanda iliyofanyika kwenye Kata ya Msamala na Kata ya Seedfarm na Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Ruvuma ambaye pia Diwani wa Kata ya Mjini Joseph Fuime ambapo katika mikutano hiyo jumla ya watu 60 walijiunga na chama hicho, ambapo kati yao viongozi wanne wa CCM kata ya Seedfarm walijivua gamba na kuvaa gwanda.

Fuime alisema kuwa Chama cha Mapinduzi kimemtuma Nape azunguke nchinzima na kuendelea kuwadanganya wananchi kwa kutoa maagizo kwa Serikali ambayo imeshindwa kuifikisha nchi kwenye ustawi stahiki miaka 50 tuka tupate uhuru.

Alisema kuwa Serikali iliyopo madarakani inaongozwa na Ccm hivyo maneno ambayo anazunguka nchi nzima kuyaongea Nape ni kuwadanganya wananchi kwani alipaswa amwagize Rais Jakaya Kikwete kwenye vikao vyao vya chama na wananchi waone utekelezaji na sio kutoa maagizo ambayo mtekelezaji wake ameshindwa toka alivyokuwa Rais mwaka 2005.

Alifafanua kuwa Serikali ya Ccm toka mwaka 2005 hadi sasa imeshindwakuwakomboa wananchi kutokana na umaskini ambao unawakabili bali kila sikuimekuwa ikiwanyang'anya uwezo wa kuyafikia maisha bora kwa kuwapandishia gharama za maisha kupitia mfumuko wa bei na wafanyabiashara wengi wamekuwa wakitoa huduma kwa Serikali na kuwacheleweshea malipo hali ambayo inaendeleza ugumu wa maisha.

Alieleza kuwa baadhi ya wafanyabiashara walihifadhi mahindi ambayo yalinunuliwa na Serikali kwenye magodauni yao na wengine waliyasafirisha mahindi hayo kutoka Songea kuyapeleka Makambako na Dar Es Salaam lakini hawajalipwa hadi leo jambo ambalo linaendelea kuwafanya wananchi wa mkoa waRuvuma ambao una viwanda vichache kuishi katika maisha magumu.

Naye Diwani wa Viti Maalumu wa Chadema Manispaa ya Songea Roda Komba alisema kuwa Chadema ndicho chama chenye dhamira ya kweliya kuwakomboa Watanzania wote katika lindi la umasikini, ujinga na maradhi hivyo wananchi kuweni makini sana na porojo za Chama cha Mapinduzi kwani hakina jambo jipya watakalowafanyia wananchi kwasababu kwa muda mrefu wamekuwa wakiwaongoza bila kuleta tija.

Komba alisema kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduziimeshindwa kuwajali wananchi ,wakiwemo wazee kwa muda mrefu kwa kushindwa kuwapatia huduma stahiki za jamii na kuwasababishia kuona maisha ya uzeeni kama ni hatari ambayo inapaswa kuogopwa.

Alisema kuwa katika nchi nyingine wazee wanaheshimika na wanapewa huduma za jamii bure ikiwemo matibabu na pensheni kwa wazee bila kujali kuwa ulifanya kazi serikali kwani mchango walioutoa katika ujenzi wa taifa walipokuwa vijana unatosha kuwaenzi wanapokuwa wazee.
 
Nape acha propaganda, waeleze watanzania ukweli.Jaman wtz sikuhizi wamepevuka wanajua mbivu na mbichi, siyo kuwadanya hovyo. Uchumi ni duni sana, nchemba na first class yake ameshindwa, amebaki kuimba ngonjera bungen km wewe nape unavyo toa ngonjera kwenye majukwaa. Polen magamba.
 
Songea amsha amsha nchimbi kashakimbia huko hana hamu tena ya kukaaa huko!!!!!!!!!!!!!!
 
kusini hakuwezi kabisa huyu bwana kule watu washagundua michanga ya macho ata mkikata umeme kwa baadhi ya sehem zilizojaa bendera za chadema poa tuu
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom