Nape apigwa dongo Mufindi

Mlyafinono

Senior Member
Apr 6, 2012
177
47
Katika mkutano wa hadhara wa nape juzi Mufindi wananchi wameonyesha kutoridhishwa na uwezo wa nape wa kujenga hoja kama wapinzani wanavyofanya.

Wananchi wamehoji kwanini habari za Nape haziandikwi kwenye magazeti kama zinavyoandikwa za CHADEMA wanapokuwa kwenye mikutano yao?

Source: ITV news leo asubuhi
 
tatizo anawapa wakati mgumu waandishi wa habari wanashindwa kuhariri maneno yake maana huwa haeleweki anaongelea nini.!
 
Ina maana kuwa kweli Uhuru na Mzalendo huyawafikii au hawayahesabu kama vyombo vya habari?
 
Labda gazeti la Uhuru linaweza kuandika habari za nape tena kwa maelekezo maalum. Gazeti makini haliwezi kuandika habari za mtu asiyeaminika. Waliandika habari ya siku 90 za kujivua gamba zilipofika akaingia mitini walipombana akageuza lugha. Hakuna gazeti linaloandika habari za aina moja mwaka mzima maana hotuba zote za Nape ni kuhusu UANAHARAKATI, KASKAZINI na DR SLAA, hajawahi kuongea tofauti, hajawahi kuongelea wanaojifungua kwenye sakafu, wanafunzi kukaa chini, malipo ya korosho, kupanda bei za bidhaa. Sasa gazeti gani litaandika habari tatu mwaka mzima
 
sasa mtu kama hana jipya zaidi ya kupiga debe lililo na kutu ataandikwa kwa lipi?
 
Hamjamsikia huwa anatoa maagizo kwa vyombo vyote vya dola ....,,,,, kisa chama chake ndiyo cyenye dola.
 
Usishangae hilo nape,ccm,cuf,ncrr wote wamepoteza dira,ikiwa magazeti yao ya uhuru na mzalendo yamewaacha na kukimbilia cdm huoni ni tabu?
 
Tatizo kubwa hana kumbukumbu na kauli zake anazo zitoa kila kona ya nchi.
 
Nape amekutana na mashwali ya msingi kutoka kwa wakazi wa mafinga na kushindwa kuyajibu, mbao zinatoka mafinga lkn wanafunzi bado wanakaa chini, mikutano ya cdm inakubalika sana na kupendwa na watu na kuandikwa sana ktk vyombo vya habari lkn ya ccm inadorola, ubadhirifu kila mahali nk.

Je kwa mwendo huu ataweza kufuta nyayo za chadema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom