Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Mgombea Ubunge katika Jimbo la Mtama mkoani Lindi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema wanaohoji utu wa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan anatakiwa kupingwa kwani amefanya mengi makubwa ikiwemo kumimina ajira kwa Watanzania katika kipindi kifupi cha uongozi wake.
Nape amesema 'utu' wa Dkt. Samia ni kielelezo tosha kinachoashiria ushindi kwa mgombea huyo kwani ameeleza kuwa Watanzania wengi wanamuelewa kutokana na maendeleo waliyoyapata katika kipindi cha uongozi wake.
Nape amesema hayo katika mkutano wa kampeni wa Dkt. Samia unaofanyika wilayani Mtama mkoani humo ambaye ananadi sera za CCM kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.