Nape amshukia Dr. Slaa kuhusu ACT- Wazalendo

Nape amshukia Dr. Slaa kuhusu ACT- Wazalendo

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,538
KATIBU wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye,amekanusha taarifa zilizopo kuwa chama hicho kinakisaidia Chama cha ACT Wazalendo akidai kuwa hawana sababu ya kufanya hivyo. Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa Nape zinasisitiza kuwa CCM hakina sababu ya kusaidia chama kingine cha siasa hivyo uvumi huo ni uchafuzi wa kisiasa.

Akizungumzia kauli ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema, Dk Wilbroad Slaa,kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanza kuandikisha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika ngome ya CCM alisema huo ni upotoshaji uliokubuhu kwani tanzania nzima ni ngome ya chama hicho.

Alisema ratiba ya NEC haijapangwa kimkakati kama alivyodai Dk Slaa na kila mtanzania ataandikishwa kwa mujibu wa sheria hivyo kauli za kuwapotosha na kuwapa hofu wananchi hazina mashiko.

"Kauli hizi za Dk Slaa mzee kama yule ni uthibitisho tosha kwamba wenzetu vyama vya upinzani hasa chadema siasa zao zina lengo la kuwagawa watu kikanda,kanda wanayoiona ni kaskazini, uthibitisho wa mbegu mbaya ya chuki," alisema Nape.

Alisema CC M wanalaani vikali siasa za namna hiyo kwani hizo sio hoja za msingi ila ni za kuwagawa wananchi na kupandikiza chuki zisizokuwa na maana na suala hilo linaonyesha jinsi wapinzani wanavyofanya siasa za kikanda.

"Tunayo taarifa kwamba Dk Slaa,Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe pamoja na Mwenyekiti wa Nccr-Mageuzi,James Mbatia walikaa vikao wakawatenga wenzao wanaunda Umoja wa Katiba Mpya (Ukawa, ambao ni Mwenyekiti wa CUF,Profesa Ibrahim Lipumba ambaye anatokea Tabora na DK Emmanuel Makaidi ambaye anatoka Kusini, hao wote tunajua wanatoka mikoa gani,"alisema Nape

Nape alisema siasa za namna hii zinazigawa nchi na kinachoonekana ni kwamba wapinzani wanajua kuwa watashindwa na ccm ndio maana wanatafta sababu,hivyo anawatoa hofu wananchi kuwa kila mtu mwenye sifaa ataandikishwa.

"Chadema wanajua watawaangusha vibaya, hatuna mpango wa kutumia mizengwe watanzania watatuchagua, waache kuwagawa watanzania kwa kutaka madaraka, wanatakiwa kuwashawishi wananchi kujiandikisha kama CCM tunavyofanya"alisema Nape

"Wanapandikiza mbegu mbaya na chuki yenye lengo la kugawa watanzania,nchi hii ni moja ina makabila 136 na tunaishi vizuri hizi siasa chafu hazifai,, maneno ya hovyo ambayo hayastahili kusemwa na mtu mzima kama yule, watashindwa ndio maana wanasema watu wanaandikishwa kiujanja ujanja, wameanza kujenga mbinu za ajabu, wananchi wanatupenda na watazidi kutuchagua,"alisema Nape

Alivitaka vyama vya siasa kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na waliache zoezi hilo liende kama lilivyopangwalilivyopangwa, wasiwajengee watu hofu, hii sio sawa.


Chanzo: Fullshangwe
 
Akizungumzia kauli ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema, Dk Wilbroad Slaa,kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanza kuandikisha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika ngome ya CCM alisema huo ni upotoshaji uliokubuhu kwani tanzania nzima ni ngome ya chama hicho.

Shutuma za uandikishaji zimetolewa kwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi...

Lakini ajabu majibu ya shutuma yatolewa na msemaji wa CCM...

Nape aache kukurupuka, kama shutuma hizo hazina ukweli akae kimya...

Walioshutumiwa watajibu...
 
Alichoongea nape ni kweli kabisa , huyu Slaa anapenda sana kulalamika
 
Jamani CCM imeshatuchosha inatakiwa tuiweke kaburini tuizike mwaka huu.Siku zilizopita Nape alisikika kwenye vyombo vya habari akimsifia Zito kua,ni mwana SIASA mashuhuri na hodari.

Pia Nape alimuomba Zito aachane na siasa alizokuwa akizifanya akiwa CHADEMA.Kwa maneno hayo ya mpuuzi Nape nidhahiri kwamba Nape alikuwa anampigia kampeni msaliti Zito na chama cha CCM B (ACT).Mpuuzi Nape hapo anakanushaje kwamba hawaisaidii CCM B(ACT)?
 
Jamaa hatumii akili akiwa kijana, sidhani kama akizeeka atabadilika, anaingilia madaraka ya NEC, au Msemaji wa CCM na NEC ni mtu mmoja?....poor Nape.
 
ukimtakafari Nape unapata picha kamili ya anaowaongoza,kwa sababu ni ngumu sana kipofu kumwongoza anayeona!!!
 
Comical Nape (Nape mchekeshaji) at his best!

Eti Watanzania wanawapenda sana CCM. Hivi anafikiri kutafuta viongozi wa nchi ni sawa na mashindano ya mapenzi!
 
Ambaye hatasema kuwa act ni kundi la ccm naye anapaswa kuitwa musaliti wa mabadiliko
 
Nape, siku zako zinahesabika ndani ya CCM...utakaa mtaani, labda uombe utuniukiwe 'bakshish' za ukuu wa vitengo au uupate ubunge endapo CCM itakuhurumia...!
Wewe Tangu lini ukawa msemaji wa ACT, AU Msemaji wa Tume? ccm itakutosa...utabaki macho wazi kama mtangulizi wako Mukama....!
Suala la kupewa tena Ukuu wa Wilaya 'zawadi' halitakuwepo tena maana CCM inaondoka madarakani na wakuu wake wa wilaya na mikoa...no more such a dubious system ever!
 
Huyu kabla hajaropoka inatakiwa amtafute baba yake wa kibailojia ni nani na yuko wapi ili amjue sio kurukia familia nyngine,akishamjua baba yake nani ndio aanze kuropoka.
 
Huyu mropokaji aka mpwayukaji anapenda kusikika kupata kick kupitia viongozi wa cdm kila neno analokuja nalo ni cdm atatiwa gundi kwenye topo lake asiongee.maana si msemaji wa act wala tume kwann ajibu

Kimbelembele niwakumpuuza na kumradhau ,watu kama hawa wanapatikana ccm tu.
 
Huyu mropokaji aka mpwayukaji anapenda kusikika kupata kick kupitia viongozi wa cdm kila neno analokuja nalo ni cdm atatiwa gundi kwenye topo lake asiongee.maana si msemaji wa act wala tume kwann ajibu

Kimbelembele niwakumpuuza na kumradhau ,watu kama hawa wanapatikana ccm tu.

Nape ni debe tupu ambalo upepo tu unalifanya lipige kelele. Msihangaike naye.
 
Tanzania tusipokaa vizuri, huyu Dogo Nape ataweza kutuletea mtafuruku mkubwa sana katika utaifa wetu. Yeye na vijana wenzake kina Ridhiwani wamekuwa wakitafisiri kila kauli, tukio na mhemuko kwa macho ya ubaguzi. Hata kama Dr Slaa alikutana na Mbowe pamoja na Mbatia, sio lazima walifanya hivyo kwa kuwa ni watu wa Kaskazini. Hakuna mbaguzi kuliko yule anayeona mwenzie kwa sura yake, dini yake, ukanda wake, jinsia yake! Hivi ndivyo amekuwa Nape, tofauti kabisa na itikadi ya CCM, chama kilichoasisi umoja na kuelea umoja wa kitaifa.

Ni mara ngapi tumejikuta watu wenye imani moja tunafanya kazi kwenye kamati moja lakini utendaji wetu hauhusiani na imani zetu, na wale uteuzi wetu hauna mkono wa imani zetu? Mara ngapi tumekuwa wapangaji kwenye nyumba wote tukiwa na asilia moja lakini ndio tumekutana mara ya kwanza na tumeendelea kuishi bila kurejea asili yetu bali kuishi kwa mnajili wa maisha tuliyo nayo? Na hata kama tumejikuta tunaishi, au kufanya kazi tukiwa mchanganyiko wa imani, itikadi, sura, jinsia au hata na aina mbalimbali ya ulemavu, je hatukuendelea na kazi bila kujali unasibu wetu? Hatuishi kama waislamu na wakristo ndani ya nyumba moja na tunavumilia na wala hatugundii kuwa kuna tofauti hizo baina yetu hadi siku tunapoachana kwenda kwenye nyumba za ibada tofauti?

Nape, Nape, Nape, kwa nini unakuwa mbaguzi kiasi hicho? Kwa nini unataka kutumia lugha laini yenye ukakasi wa kututenganisha? Unaweza kweli kushuhudia hizo dhamira ulizowawekea Mbatia, Mbowe na Slaa eti wamewatenga wenzao Lipumba na Makaidi. Please wewe ni zaidi ya hapo. Hukui tu! Sitaki nikutukane mjinga, ila tafadhali usije ukawa sababu ya machafuko nchini. Vijana na watoto wanakusoma!
 
Nape ni debe tupu ambalo upepo tu unalifanya lipige kelele. Msihangaike naye.

Hapana Hatuwezi kumwacha! Anamwaga chumvi ya uchochezi katika jamii. Ana kundi kubwa la watu nyuma yake. Na kwa namna hii Nape ataleta vita ya kiukanda nchini. Tungekuwa na serikali makini, Nape angepaswa awekewe mashtaka ya uchochezi. Nape ni hatari kwa taifa hili, huwezi ukamwacha aendelee kubwata bwata kama anavyofanya. Kauli zake ni za kipuuzi lakini tofauti na mimi na ninyi, yeye amepewa kundi la kumsikiliza na anafanya hivyo kwa jina la chama kikubwa, chama kilichoaminiwa kwa zaidi ya umri wa wanaomfuata. Hapana si wa kupuuza. Ni wa kusweka ndani na kunyamazishwa. CCM Vipi INALALA USINGIZI MNONO WAKATI MISINGI ILE IMARA YA MWASISI WAKE IKINOFULIWA KINOMA!?
 
Back
Top Bottom