VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Kwa 'kutumbuliwa' kwa aliyekuwa Waziri wa Habari Nape Nnauye ni dhahiri kumzuia asiikabidhi Ripoti ya Kamati Maalum ya kuchunguza uvamizi wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Daudi Albert Bashite alias Paul Makonda. Ni kwakuwa Nape aliahidi wananchi kuwa ataikabidhi Ripoti hiyo, akiwa kama Waziri, kwa Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na kwa Rais.
Mdogo wangu Nape Nnauye, historia itakulinda. Umetekeleza wajibu wako. Ujumbe uliopo kwenye Ripoti walishaupata. Ujumbe ulishawafikia. Anayelindwa na anayewindwa wote watakatazwa na muda. Muda utaamua. Nape, umeponzwa na kuwa 'kiongozi'. Ulipaswa kuwa mtawala. Pole.
Kwa kazi kubwa uliyoifanya na Komredi Kinana, hukupaswa 'kutumbuliwa' kirahisi hivyo. Unatumbuliwa kwa kutenda kazi yako? Kisa ndiye huyu DAB alias PCM? Inasikitisha. Lakini, yote ni maisha. Kubali kilichotokea na uwatumikie wananchi wako wa Mtama. Nasema tena, amini nawaambia, Nape atalindwa na historia katika kutetea tasnia ya habari.
Mwafaaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam