Nape adai kunasa nyaraka za Marando | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape adai kunasa nyaraka za Marando

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by engmtolera, Jun 4, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amedai kuwa amenasa barua za mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mabere Marando, akikana kuwaambia Watanzania kuwa yeye (Nnauye) alifaidika na fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania.

  Nape aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza katika mkutano mkubwa wa hadhara, uliofanyika mjini Mpanda, mkoani Rukwa na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa mji huo na vitongoji vyake.

  "Kimsingi namheshimu sana Marando, lakini kitendo cha kuchanganya uwakili na siasa karibuni kitamgharimu, hasa siasa za majitaka za Chadema," alisema Nape huku akishangiliwa na mamia ya wananchi waliofurika katika mkutano huo.

  Alisema kufuatia hatua yake ya kupata ushahidi wa nyaraka, anamtaka Marando kuchagua ama kufanya siasa au kuendelea na kazi yake ya uwakili kwa sababu kufanya vyote kwa pamoja kutamgharimu.

  Nape alisema madai ya Marando dhidi yake, aliyatoa hivi karibu baada ya yeye kumtaka Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilibrod Slaa, aache unafiki kwa kueleza sababu za kulipwa na chama chake Sh 7.5 milioni kila mwezi tena bila kuzilipia kodi.

  Alisema rai yake wa Dk Slaa, ilitokana na ukweli kwamba aliwahi kupinga wabunge kulipwa mshahara usiofikia kiasi hicho kwa kwa maelezo kuwa ni mkubwa.

  Alisema badala ya raia hiyo kujibu na Dk Slaa, Chadema ilimtumia Marando ambaye alitoa tuhuma kwamba Nape ni miongoni mwa waliofaidika na fedha za EPA wa msingi huo ni mmoja wa mafisadi.

  Kwa mujibu wa Nape, katika madai yake Marando alidai kuwa yeye (Nape) alipewa fedha hizo za wizi na mfanyabiashara mmoja wa jijini Dar es Salaam.

  "Nilishituka sana kusikia mtu ninayemheshimu akitoa tuhuma hizo mzito, nikajua ndio matatizo ya kuchanganya siasa na uwakili, siasa zenyewe za Chadema. Lakini cha ajabu baada ya siku chache Marando amemwandikia mfanyabiashara huo, akikanusha taarifa ile na kuisukumia Chadema,"alisema Nape.

  "Nadhani ni muhimu Marando akachagua kufanya siasa au kuendelea na kazi yake ya uwakili kabla aibu kubwa haijamkuta," alisistiza.

  Akionyesha kujiamini kuwa ana nyakaraka za uthibitisho, Nape alisema anazo barua za mawasiliano kati ya mfanyabiashara huyo na Marando, zinazoonyesha wakili huyo alikataa katakata kuhusika na kauli iliyonukuliwa kwenye vyombo vya habari.

  Kwa mujibu wa Nape barua hizo ni pamoja na ya Mei 16 mwaka huu iliyoandikwa na mfanyabiashara huyo kwenda kwa Marando ikimtaka aeleze sababu za kumhusisha naye katika tuhuma za fedha za EPA.

  "Wananchi yapo mengi kama hili ambayo viongozi wa Chadema wanawadanganyeni kupitia kwenye mikutano au vyombo vya habari, lakini kwa kutojua baadhi yenu huwa mnawaami . Kitendo hiki kinamfanya Marando na chama chake wasiaminike kwa umma," alidai.

  Nape alisema, bila aibu Marando anamkana Antoni Komu na chama kuwa hakuunga mkono tuhuma hizo dhidi yake.
   
 2. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #2
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,454
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Mbona hajatoa huo uthibitisho/ Nyaraka anazaodai kama CHADEMA wanavyofanyaga.
  Hili ni gazeti gani umenukuu,nachelea litakuwa ni UHURU.
  Otherwise this is CRAP
   
 3. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuuu porojo hizo
   
 4. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nape inabidi ukubali tuhuma, umakini wa CDM ndio leo unawafanya mnawaita wenzenu mafisadi. List ya mwembe Yanga ndio mnahangaika nayo. Huwezi kujinasua kwa hilo, wewe ndio unatakiwa utueleze kwanini ulishiriki kula fedha za wizi za wavuja jasho amaboa leo hujui uwaaambie nini.

  Umakini wa CDM umewafanya CCM inaimba wimbo wa CDM. Kijana Nape kama mmemtumia mfanyabiashara mnayempeleka puta kwa fedha mlizogawana ili awasaidie kusema eti yaliyosemwa sio unajikaanga. Mfanyabiashara ambaye unasema umepata barua hiyo ndiyo aliokupatia mgawo baada ya kukamilisha ukwapuaji, leo anahaha mahakamani unafikiri atafanya nini, fedha mmekula ninyi zigo mmemwachia.

  Niliwahi kuzungumza na wakili wake wa kwanza kabla ya Marando aliweka vizuri sana jinsi mlivyogawana zile fedha, huku baadhi zilitumika kununulia magari ya CCM kutoka india. Na wengi mlikula ule mgao kwa njia tofauti. kama kweli ile kesi ikienda mahakamani vizuri, Nape na wengine wengi mtaitwa ili kutoa maelezo ya mgawo ulivyokwenda.
   
 5. MachoMakavu

  MachoMakavu JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  porojo zikiendelea!
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  Nape ana janaba la fikra
   
 7. J

  JACOBUDA Member

  #7
  Jun 4, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ingekuwa vizuri na yeye marando akatoa vithibitisho
   
 8. u

  urasa JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nape hajamalizana na mapcha watatu anarukia kwa chadema,ngoja lowassa aanze kumshughulikia huyu nape,anadhani ukimya wa lowassa una maana gani?
   
 9. W

  Wavizangila Member

  #9
  Jun 4, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nape zungumzia mahitaji yetu ya msingi banaaa, hata hivyo mmefikia wapi na three pachaz na wale wanachama wa ccm wanaodaiwa kuanzisha ccj mumo kwa mumo. Twambiee dogo.
   
Loading...