NAPE: 60% ya Muziki utakaochezwa katika vyombo vya habari lazima uwe wa nyumbani

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Wakati baadhi ya wasanii na wadau mbalimbali wa burudani nchini wakiendelea kuwa na hofu juu ya mfumo mpya unaovitaka vituo vya redio na runinga kuwalipa wasanii mirahaba inayotokana na kucheza kazi zao, serikali imesema imeunda sheria ambayo itavifanya vishindwe kuepuka kucheza nyimbo za wasanii wa ndani.

Akizungumza na Bongo5 Jumanne hii kwenye uzinduzi wa filamu ya ‘Home Coming’ Mlimani City jijini Dar es Salaam, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye alisema sheria hiyo inazitaka TV na Redio zenye vipindi vya burudani kuhakikisha 60% ya content ni ya nyumbani.

“Tumeshatangaza kuanzia tarehe moja mwezi wa kwanza 2016 kila muziki wa msanii utakaopigwa kwenye redio ma television utalipiwa,” alisema.

Sheria ilishasainiwa na tumekubaliana na watu wa COSOTA wataisimamia na tumeweka kampuni ya kusimamia muziki umepiga mara ngapi na TV gani.”

“Mimi nataka watu waniamini historia yangu, waamini watu watalipwa na haki yao wataipata na jasho lao watalipata. Nilichowaambia kila jambo jipya lazima litakuwa na mapungufu ila sheria ndio zitatuongoza, kila redio na TV zenye vipindi vya burudani wanatakiwa kuhakikisha 60% ya content wanayoitoa iwe ya nyumbani, hakuna wakukwepa hili,” alisisitiza Nape.

Pia Nape alisema tayari ameshakaa na wahusika wa nyombo vya habari na kuzungumzia namna ya utekelezaji wa suala hilo.

“Vyombo vya habari ndio wamekuwa wakinisukuma kufanya hivyo, kwahiyo kama wao ndio wameamua hivyo sisi ulikuwa ni utekelezaji na naamini kila kitu kitaenda sawa.”

Chanzo: Bongo5
 
Last edited by a moderator:
MIMI NAONA SERIKALI HII YA AWAMU YA 5 INAINGILIA SANA SEKTA BINAFSI, UKIANGALIA HII YA RADIO/TV PAMOJA NA ILE YA SHULE BINAFSI KUPANGIWA ADA, AISEE INAINGILIA SANA
 
Kwani lazima radio stations zipige miziki? Wakiamua kudesign programs za kuelimisha au kustorisha tu mwanzo mwisho, si ndo wasanii watakosa platform kabisa? Mifano ya stations kama hizo ipo Aljeera, CNN, RT etc hamna miziki kule.
 
Ninachokiona taratibu Serikali inakosa mwelekeo!. Kwa kujisahau au kwa makusidi kuwa tuko Biashara huru/huria na kwamba soko ndiyo nguvu yetu!.

Serikali makini huja na sera mbadala ya kisoko na siyo ubabe kwenye Biashara za watu.

Mfano nilitegemea Waziri angekuwa anasema kwamba Wizara yake itaipatia nafuu kadhaa Redio na TV itakayojali Music na Wanamusiki wa Nyumbani!.Kinyume na hapo nao taratibu mkono wa Chuma unataka kutumika kuzizika Tv za Watu Binafsi na kubakiza TBCCCM
 
okay nimefanya research na kuona wateja wangu wanapendelea charanga na western music..., Je nipoteze hao wateja sababu tu ya kuridhisha matakwa ya Waziri ?

Tuache kupangiana interest na kulazimishana jinsi ya kufanya biashara, huu sio uzalendo bali ni udikteta
 
Kwani sasa hivi muziki wa nyumbani si unachezwa kwa zaidi ya 70%?

Au yeye kwenye gari yake na nyumbani anasikiliza nyimbo za Komba tu?
 
Hapo ni ukandamizaji
Tena mkubwa sana,maana mziki wa nyumbani ni kama mnanda, sindimba, mdumange, mchiriku,segere.
sasa kweli utaweka miziki hiyo 60 % kisha hiyo biashara utafanya na wamakonde wauza vinyago pale mwenge.
 
Last edited:
Mimi nadhani hizo media (TV na Radio) zitumie furusa hiyo kukuza biashara yake...hakuna haja ya kulalamika. Buni mbinu yakuhakikisha unapata faida mara dufu kwa kutumia furusa hii ambayo serikali uimeitoa....! Jambo la kwanza anza kuwahimiza wanamuziki wetu kutengeneza muziki wenye ubora wa hali ya juu ambao utawalazimisha wananchi wote nchini , nchi za jirani, na duniani kwa ujumla kukimbilia kusikiliza muziki wa wawatanzania....! maana watakuwa na uhakikia wa kusikiliza muziki huo kwa asilimia 60%...zipo mbinu nyingine nyingi za kutumia furusa hii iliyotangazwa na Waziri wa Mh. Magufuli.

Tuache kulalamika tutumie fursa hii sasa.
 
Huu mziki usipigwe kabisa kuwe na vipindi vya hotuba za marais wa kwanza wa Afrika kuanzia akina kwameh nkruma..... Samora Moses machell ,,, tafawa balewa modibo keita akina neto ,,,na wale watu maarufu like Bantu Steve bike, Walter sisul dedan kimath...... wanauchumi mbali.. Wanasayansi wachukue asilimia tisini za media.. Asilimia zilizobakia ni kumwomba Mungu na vipindi vya kumsifu Mungu
 
Back
Top Bottom