Napatwa na wasiwasi, je huyo fisadi hawezi kuwa ni mmoja kati ya wale?

marveljt

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
1,503
1,479
Kipindi akiwa CCM sisi CHADEMA tulisema ni fisadi mkuu chini ya katibu yetu ila mtuhumiwa alitoa kauli moja mwenye ushahidi aende mahakamani. Sisi CHADEMA hatukwenda inamaana ilikuwa ni propaganda. Baada ya hapo akahamia CHADEMA CCM wakasema afadhali kwani fisadi kahamia nyumba nyingine na yeye akarejea nendeni mahakamani.

Baada ya uchaguzi kuisha mkuu wa nchi si zaidi ya mara moja amesema nchi hii iko hapa kutokana na mafisadi pamoja na wajizi. Hivyo atafungua mahakama ya mafisadi. Nilitegemea kuwa yule ambaye CCM pamoja na CHADEMA walimnyooshea kidole angepelekwa huko la hasha hakuna lililotokea.

Sasa je huyo fisadi hawezi kuwa ni mmoja kati ya wale ....... Na je hakuna uhusiano uliopo na wale tulioambiwa makaburi yakifukuliwa mengine hayawezekani kufukiwa? Kama ndiye CHADEMA amefata nini?
 
Nimeanza kuamini kuwa Watanzania wengi ni wagonjwa wa akiri.huyu nae ni walewale
 
Maswali mengine kabla hujajiuliza, tafuta humu utakuta nyuzi nyingi za maswali yako. Utapata majibu zaidi ya haya.

Kila la kheri, marveljt.
 
Kinacho msumbua sijui nini ebu amwache dakta afanye kazi zake taratibu miaka mitano bado
Dr wa vyeti feki ana PhD wkt hata kizungu hajui na kumbe anaogopa kwenda nje sababu hajui akaongee nini huko Ulaya hakuna wazaramu
 
Kinacho msumbua sijui nini ebu amwache dakta afanye kazi zake taratibu miaka mitano bado
Kazi zipi? Kama sheria ni msumeno mbona uko butu? Mliogopa kumpeleka mahakamani kisa yuko ndani kwenu leo katoka nje kwa nini msimkamate? Kama mnashindwa kumkamata maana yake hamuwezi kupambana na mafisadi.haiwezekani mumtuhumi ni fisadi ili hali polisi mnao,mahakama mnazo,mahakimu mnao,majaji wenu,mahabusu mnazo,magereza mnayo. Acheni unafiki kama kweli mnapigania haki za watu wa chini pambaneni pia na hao wakubwa.au mnaogopa kijichimbia makaburi wenyewe? " msema kweli mpenzi wa Mungu" je kama unadanganya ni mpenzi wa nani?
 
Dr wa vyeti feki ana PhD wkt hata kizungu hajui na kumbe anaogopa kwenda nje sababu hajui akaongee nini huko Ulaya hakuna wazaramu

Nakuunga mkono kwa kiasi fulani kutokana na mfumo wetu wa elimu ulivyo ila si lazima kila kiongozi ajue kizungu. Mfano putin anaongea kirusi kwa vile wamejitosheleza. Hivyo na sisi baadae tukijitosheleza tunaweza kuongea lugha yetu popote
 
Back
Top Bottom