Naota nimeolewa na mtoto mdogo

Naota nimeolewa na mtoto mdogo

karma alvin

Member
Joined
Jan 9, 2013
Posts
51
Reaction score
8
Habari wa jamii,

Mimi kuna ndoto inanisumbua imekuwa ikijirudia na nikama kamuendelezo fulani hivi:

Naota nimeolewa na mtoto mdogo kabisa au mara nyingine naota nipo kwenye mahaba na mtoto mdogo.Sasa sijui hii ndoto inaashiria nini maana nimeshindwa kuielewa.

Naomba tafadhali anaejua kutafsiri ndoto anisaidie
 
ni kweli umeolewa na spiritual husband....unahitaji ukombozi..
 
Kwani umeshaolewa? na kama bado mpenz wako tofaut yenu ya umri ikoje?
 
Kumbuka huyo mtoto utakae muota huwa anatabia gani.Ila navyohisi utakuja kuolewa na mtu ambae umempita umri, kumbuka yawezekana ukawa na wako tayari unaempenda, na labda kakupita umri.But yawezekana msifike mbali, na huyo uliempita umri atakuja,
Mtafall n luv, na mtaoana.
 
Usihofu nilwahi kusoma kitabu kimoja cha dictionary of dream by ibn sirin. Ukiota upo kwenye love na mtu maana yake ni kuwa "utaingia katika biashara na mtu huyo". Lakini kwa ndoto yako inaonyesha biashara hiyo itakuwa endelevu na yenye manufaa. Hakuna mapenzi hapo.
 
Utaolewa na mtu mpole na mnyenyekevu na mwaminifu hongera sana mdada

Unaweza kutabasamu kwa mema na mazuri uyakumbukayo
 
Sina hakika na imani yako, ila hayo ni mambo ya kiimani sana.

Kuna mashetani ya mahaba huwa yanawatumia watu kutimiza haja zao hasa yakikupenda.

Ili litimize matakwa yake hua unaingia mkataba nalo bila wewe kujua, na moja ya sign tayari lilishakuvaa ni ndoto za kujrudiarudia kuhusu kitendo kinachoendelea.

Kama unaweza kaa vizuri na Mungu au watafte watumishi wa Mungu wakusaidie.

Kama huamini kwa sasa, siku utakuja kugutuka itakua too late. Maana moja ya madhara ni kukufanya usiolewe kama hujaolewa, na kama umeolewa basi kukuharibia ndoa yako kwa kukufanya usifurahie kuwa na mumeo au kukuachanisha kabisa naana huwa yanaona wivu.

The choice is yours now!!
 
karma alvin

Hey dear kama hio ndoto unaota sanaa na kukurudia..pls unaitaji kutibiwa utakuwa na jini mahaba ndo wanatabia hio ya kuoyesha mtu unafanya mapenzi
 
Last edited by a moderator:
Hilo ni pepo ua jini mahaba. Ukiwa katika hali hiyo kuolewa siyo rahisi, hata ikitokea umeolewa sahau kupata watoto.
 
Kwani ndoto yako ilishawaho kuwa ya kweli?
 
Back
Top Bottom