Masalu Jacob
JF-Expert Member
- Jul 26, 2017
- 948
- 1,092
Habari Tanzania.
Napenda kuongea na Serikali kuhusu tatizo la ajira nchini. Serikali na wadau wachache wamekuwa wakihimiza sana vijana wajiajiri baada ya kuhitimu vyuo vikuu nk. (Hawa ndio haswa wahanga wa tatizo hili kwa asilimia kubwa kutokana na mfumo husika wa elimu yetu).
1. Hivi Serikali mnakumbuka wazo na lengo lililopelekea kuanzishwa kwa taasisi ya VETA hapa nchini? Au pengine hamjui?
2. Hivi Serikali mnajua wazo na lengo mahususi la kuanzishwa mitihani ya darasa la nne, darasa la saba, kidato cha pili, kidato cha nne na kidato cha sita hapa nchini? Au mnadhani ni utaratibu umejikuta upo katika elimu yetu baada ya kuukopa mahali?
3. Hivi Serikali mnajua wazo na lengo la kuanzishwa vyuo vya kati na vyuo vikuu katika taifa la Tanzania? Au mnadhani ni fashion baada ya kuona baadhi ya viongozi waliokuwepo madarakani enzi hizo watoto wao kutokukidhi matakwa na kukosa sifa katika mfumo husika ndio tatizo lilipoanzia? Sijui kama mnajua haya mambo lakini?
4. Sijui mnakumbuka tatizo lililojitokeza kuhusu mahakama za mwanzo na wilaya kuhusu chuo cha Sheria Lushoto Tanga na janga la wahitimu wa shahada ya Sheria hapa nchini? Sijui kipindi cha awamu ya Nne kurudi nyuma mlipojadili bungeni hivi hamkuona hili tatizo kwa fani nyingine? Ubaya wote mlikuwepo.
5. Je, mlishafanya tafiti kuhusu uhitaji wa elimu ya shahada na shahada ya uzamivu kama zina umuhimu hapa Afrika sio Tanzania tu au tunaona fashion kuitwa wasomi nk?
NB:
Nawaomba sana mtafute taarifa na maarifa ya miaka ya nyuma tangu nchi inapata Uhuru viongozi waliopita walifanya nini mazuri mtakuwa na mwanzo mzuri wa kujifunza. Agalo la kale ni kinga kwa agano jipya.
Serikali yoyote hapa duniani ni kama mfano wa siku tu maana jinsi ilivyo leo inakuja na kesho inaenda zake. Siku iliyo nzuri ya kuikumbuka ni ile iliyokupa alama nzuri sana maishani mwako.