Naona Kifo cha CCM kwa Mbaaaali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naona Kifo cha CCM kwa Mbaaaali

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mlachake, Jul 30, 2010.

 1. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,924
  Likes Received: 633
  Trophy Points: 280
  GREEN DARD WA CCM IRINGA MJINI WANATUMIWA NA WAGOMBEA KUIVURUGA CCM

  [​IMG]
  Katibu mtendaji wa Club ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa Bw Frank Leonard jana amezingirwa na vijana wasiojua hata sheria moja ya ulinzi waliojipachika jina la Green Gard wa CCM katika wilaya ya Iringa mjini ambao wamekuwa kero kubwa katika kampeni za ubunge CCM jimbo la Iringa mjini.(pichani ni mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini MwlChelestino Mofuga akirejesha fomu ya ubunge hivi karibuni)

  Green Gard hao kama wanavyojiita wao walimzuia mwanahari huyo kuchukua matukio katika mkutano wa kampeni za ubunge jimbo hilo la Iringa mjini huku wakidai kuwa wametumwa na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Bw Abed Kiponza na katibu wake Otyatya kuwabana waandishi wa habari wasifike katika kampeni hizo .  pamoja na kumzuia katibu huyo tayari hadi sasa vijana hao waliojipachika majina yasiyo yao ya ugreen Gard wameendelea kuwatisha hata baadhi ya wana CCM ambao wameonyesha kutofautina na wagombea wao wanaowapigia debe ambao hata hivyo hawakubaliki mbele ya wana CCM wenye utashi .  Kundi hilo la vijana hao waliogeuka oba omba katika kampeni hizo kwa kivuli cha kulinda amani katika mikutano hiyo limekuwa likitumiwa na mgombea mmoja wa nafasi hiyo kuchana abango ya wagombea wengine pamoja na kumsemea vibaya mbunge aliyeko madarakani Monica Mbenga kama huku wqakitambua wazi mbungea wao huyo pamoja na kuwa kada mzuri wa CCM bado hana nguvu ya kisiasa zaidi ya ile ya kuchana mabango ya wenzake na kuendesha siasa za ukabila kwa kuwatumia wafanyabiashara wa mjini hapa ambao ni kabila la kwake.

  Wachambuzi wa masuala ya siasa mjini Iringa wanasema kuwa siasa zinazofanywa na mgombea Fadhil Ngajilo kwa kuwatumia wapambe wake kuchana mabango ya wagombea wenzake zinaweza kumweka pabaya kiasiasa na anaweza kuambulia patupu katika mchakato huo baada ya wana CCM kubaini mchezo huo mchafu anaocheza mgombea huyo ambaye ni mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa.  Pia wadai kuwa mbali ya memyekiti wa CCM wilaya Bw.Kiponza kudaiwa kuliunga mkono na kulituma kundi hilo la Green Gard kuwafukuza waandishi kuandika habari za CCM katika kampeni hizo bado mwenyekiti huyo wa UVCCM mkoa ameakuwa akihusika kuwatumia vijana hao kufanya fujo na kuwasema vibaya wagombea wenzake .  Kwa kuwa lengo la vyombo vya habari ni kuhabaisha umma ni wakati umefika sasa kwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa Bi.Mary Tesha kusimama na kupaza sauti ya onyo kwa Green Gard hao ambao wamegeuka vibaka katika kampeni hizo hata kuwanyanya kwa vitisho wana CCM wanaotak kuhoji maswali wagombea hao pamoja na wanahabari wanaofika kuwapima wagombea na kutoa habari zao.  Kwa maelezo yanayotofautiana ya vibaka hao katika kampeni waliojipa jina la Green Gard ni kwamba wamekuwa wakilipwa fedha za ulinzi na mmoja wa wagombea wa ubunge na ndie ambao wamekuwa wakimsikiliza na wamekuwa wakimfuata mgombea huyo baada ya CCM kushindwa kuwapa posho zao na hivyo akumua kuomba wao kwa wagombea japo ni rushwa kufanya hivyo.


  Tukio la waandishi wa habari kujfukuzwa ni la pili ambapo tukio kama hilo la katibu kufukuwa liliwakuta wanahabari wa kituo cha IMTV ambao pia walizuiwa kupiga picha na kutakiwa kuondoka katika mkutano huo japo katibu wa CCM mkoa na Kiponza kwa nyakati tofauti waliwaomba radhi wanahabai japo hawakuwakanya vijana wao waliojipachika jina la Green gard .
   
Loading...