Naona 'Kenge' Wameanza Kujitambua

Naona 'Kenge' Wameanza Kujitambua

Burkinabe

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2023
Posts
2,752
Reaction score
4,800
Habari wana jukwaa.
Ni matarajio yangu kuwa mnaendelea vyema.

Leo katika kufuatilia kwangu kile kinachoendelea kwenye harakati za kuwapata wabunge na madiwani ndani ya chama tawala, nimefurahishwa na baadhi ya wananchi wa baadhi ya maeneo hapa kwa jinsi wanavyoonesha 'reaction' kwa waliokuwa wawakilishi wao na wanataka kuendelea kuwawakilisha!

Hawa hawa waliokuwa wanawaita wananchi wao "Kenge", eti wanataka waendelee kuaminiwa na wananchi ili wakishapata tena waendeleze matusi yao kwa raia. Hapana. Hili halikubaliki kabisa. Ndiyo maana wananchi wa baadhi ya sehemu binafsi wamenifurahisha sana.

Viongozi wote wanapaswa kufahamu kwamba nguvu yao inatoka kwa hao wanaowaita Kenge. Hili linapaswa kueleweka vizuri kabisa kuanzia ngazi ya chini kabisa ya mjumbe wa mtaa hadi kwa Rais.

Unafiki wa kuwapenda "kenge" wakati wa kutafuta kura zao, hatutaki.

Tunamtaka kiongozi kama Hayati JPM ambaye kamwe hakuweza kuacha kusikiliza wanyonge (kenge) kwenye mikutano yake.

Hatutaki kiongozi ambaye hakutaka kuwasikiliza wanyonge wakati wa kipindi chake cha urithi (ushahidi upo).

Hatutaki viongozi wenye kaliba ya "mama wa kambo".

Wananchi wa Butiama mmenifurahisha sana.

Hili naomba lisiishie Butiama tu, liende pote palipokuwa na viongozi wa hovyo waliowaona wananchi wao kama "Kenge" tu.

Sasa wakati wa kenge kuonesha umuhimu wao, umefika.

NOTE:
Mh. Balozi Polepole, shikilia hapo hapo, tuko pamoja na wewe.

Mungu ibariki Tanzania
 
Butiama ina umuhimu wa pekee kwa nchi yetu kwa sababu ni sehemu alikotokea Baba wa Taifa.
Baba wa Taifa alikuwa mpenda haki.
Baba wa Taifa hakuwa mnafiki.
Baba wa Taifa hakuwa kujilimbikizia mali.
Baba wa Taifa hakuwatweza watu wake.
Baba wa Taifa hakupendelea watoto wala familia yake kuwapa nafasi wasizostahili serikalini.
Baba wa Taifa alijichanganya na wananchi wa hali ya chini ambao ndio walio wengi nchi hii.
 
HIvi yule madame alietuita kenge pale bungeni yupo kwenye kuomba kura.? Ili tumkumbushe
 
Butiama ina umuhimu wa pekee kwa nchi yetu kwa sababu ni sehemu alikotokea Baba wa Taifa.
Baba wa Taifa alikuwa mpenda haki.
Baba wa Taifa hakuwa mnafiki.
Baba wa Taifa hakuwa kujilimbikizia mali.
Baba wa Taifa hakuwatweza watu wake.
Baba wa Taifa hakupendelea watoto wala familia yake kuwapa nafasi wasizostahili serikalini.
Baba wa Taifa alijichanganya na wananchi wa hali ya chini ambao ndio walio wengi nchi hii.
Toa upuuzi hayo yote yanatokea Tanzania ni misingi yake sijui una umri gani wewe Nyerere alikuwa dikteta na mbaguzi.
 
Mkuu usiwaamini sana watu, unaweza kushangaa huyo anaezomewa hapo ndo akashinda tena kwa kura nyingi sana!
 
Miaka mingi tu wananchi washaanza kujielewa tatizo Tanzania mwananchi hamchagui kiongozi yoyote ni watu wa kupitisha tu mfumo ulichoamua
 
Habari wana jukwaa.
Ni matarajio yangu kuwa mnaendelea vyema.

Leo katika kufuatilia kwangu kile kinachoendelea kwenye harakati za kuwapata wabunge na madiwani ndani ya chama tawala, nimefurahishwa na baadhi ya wananchi wa baadhi ya maeneo hapa kwa jinsi wanavyoonesha 'reaction' kwa waliokuwa wawakilishi wao na wanataka kuendelea kuwawakilisha!

Hawa hawa waliokuwa wanawaita wananchi wao "Kenge", eti wanataka waendelee kuaminiwa na wananchi ili wakishapata tena waendeleze matusi yao kwa raia. Hapana. Hili halikubaliki kabisa. Ndiyo maana wananchi wa baadhi ya sehemu binafsi wamenifurahisha sana.

Viongozi wote wanapaswa kufahamu kwamba nguvu yao inatoka kwa hao wanaowaita Kenge. Hili linapaswa kueleweka vizuri kabisa kuanzia ngazi ya chini kabisa ya mjumbe wa mtaa hadi kwa Rais.

Unafiki wa kuwapenda "kenge" wakati wa kutafuta kura zao, hatutaki.

Tunamtaka kiongozi kama Hayati JPM ambaye kamwe hakuweza kuacha kusikiliza wanyonge (kenge) kwenye mikutano yake.

Hatutaki kiongozi ambaye hakutaka kuwasikiliza wanyonge wakati wa kipindi chake cha urithi (ushahidi upo).

Hatutaki viongozi wenye kaliba ya "mama wa kambo".

Wananchi wa Butiama mmenifurahisha sana.

Hili naomba lisiishie Butiama tu, liende pote palipokuwa na viongozi wa hovyo waliowaona wananchi wao kama "Kenge" tu.

Sasa wakati wa kenge kuonesha umuhimu wao, umefika.

NOTE:
Mh. Balozi Polepole, shikilia hapo hapo, tuko pamoja na wewe.

Mungu ibariki Tanzania
View attachment 3427766
Butiama mpo vizuri tunataka kama hi yo
 
Back
Top Bottom