Naona dalili zote za kuwa mganga

Mkondo wa Nungwi

JF-Expert Member
Feb 16, 2019
332
383
Nilileta thread hapa niliwahi kumiliki maduka 11 lakin sasa nimefilisika.

Kwa kweli sikuwahi kumfikiria yoyote ubaya na hesabu zilikua zinakwenda uzuri ingawa wengi wasiojua sababu ya kufisika wanakuona mzembe lakin wajiulize kama ulianza chini ukafika juu uzembe huo unatokea wapi?

Kuna thread nilisoma humu nguvu inayokumiliki ndio sababu ya kufanikiwa kwako au kuharikiwa ingawa wengi wanalaumu kurogwa.

Mimi nimefilisiwa na nguvu inayonimiliki ikiwa ni aina yoyote kutoka kwa mungu ama shetani au yoyote.

Nilijiuliza tu nilifanya kosa gani mpaka nikafilisika hadi naomba nauli lakin sasa dalili naziona dalili za kusoma sana thread za magojwa humu na pia nikichat na watu naweza kuanza kumwambia mambo yake.

Mzee wangu alibahatia kuuza nyumba alitaka kunipa pesa nyingi nirud kwenye biashara lakin cha kushangaza nazungumza nae kichwa kilifanya kuzunguka kama kinakataa zile pesa kweli hakunipa tena pesa na sina popote nunakofikiria kupata tena pesa za kurudi kwenye mzunguko wa biashara ambayo ndio ilikua ndio niliokulia nayo tangu mdogo.

Najiuliza kuna sababu gani wengi waliopitia kufilisika na maisha baadae wanakua waganga je hii funny haitakiwi kumiliki asset na kumiliki biashara na maisha yakaendelea.

Kama yupo wa kunisaidia nijitoe kwenye hili asaidie sijaipenda kabisa hii ya kutaka kutoa tiba ingawa nimeona dalili za tiba itakua ni kusomea maji na mimi huko nyuma niliwahi kufanyiwa kama hiyo pahali ikanisaidia sana.

Nguvu kubwa ipo iliyonimiliki mwilini mwangu na nimegundua ilinianza tangu mdogo kwasababu sikuwahi kupata utulivu wa fikra kama ninazozihisi sasa hivi muda mrefu baada ya kufilisika.

Sasaivi ni kama ninataka kubadilishwa maisha yangu na nguvu hii iliyoniweka kitako tangu mwaka 2015 mpk saiv naendelea.
 
Anza kwa kufunga akaunti zako za wasapu, fesibuku, insta na nyingine ulizokuwa ukijidai na kujitanua nazo, halafu tafakari uhusiano wako na yale makundi uliyoyapa mgongo.
 
Anza kwa kufunga akaunti zako za wasapu, fesibuku, insta na nyingine ulizokuwa ukijidai na kujitanua nazo, halafu tafakari uhusiano wako na yale makundi uliyoyapa mgongo.
Nilitafakari kufunga akaunti zote nikipata shuhuli ya kufanya mkuu na sikuwa na makundi kabisa
 
Chagua moja tu kati ya haya maoni yangu mawili hapa chini;

1.) Mrudie Muumba wako kwa moyo wako wote na akili zako zote! na hivyo kuachana kabisa na hayo mawazo/imani potofu iliyo tapakaa kichwani mwako.

2.) Njoo haraka Tanga ili nikupeleke Kijiji cha Kwa Msisi ili ukapewe matunguri ya kukulinda kwenye hizo biashara zako.
 
Sina biashara tena mkuu soma vizuri
 
Back
Top Bottom