Naona Dalili za CCM kubadili mgombea Chalinze

Naona Dalili za CCM kubadili mgombea Chalinze

Siku kadhaa baada ya CCM kupata mgombea ubunge Chalinze,imeonekana kijana huyu amechafuka chapa chapa na kashfa za ufisadi.Kila kukicha zimekuwa zikiporomoshwa kashfa kubwa na ndogo akihusishwa kijana huyu.Watu waliopewa jukumu kumuuza wanahaha jinsi ya kumsafisha. SWALI:Nani wa kumtawadha huyu mgombea

rizwani ana pesa kushinda wachaga wote kwa pamoja .safi sana riz mwanaume pesa shikamoo kelele tu
 
Hehehehehe wacha nicheke mie niongeze week za kuishi
 
Kwa kikwete alivyo wote watapata madaraka makubwa kuanzia ubunge wa riz,uku wa wilaya,rc,katibu wa wizara,wakurugenzi wizarani.cha msingi atahakikisha wanabadilisha majina
 
kuna jamaa mmoja humu ndan ncmtaj ni mtt wa kikwete, cjui nimtaje...?
 
Siku kadhaa baada ya CCM kupata mgombea ubunge Chalinze,imeonekana kijana huyu amechafuka chapa chapa na kashfa za ufisadi.Kila kukicha zimekuwa zikiporomoshwa kashfa kubwa na ndogo akihusishwa kijana huyu.Watu waliopewa jukumu kumuuza wanahaha jinsi ya kumsafisha. SWALI:Nani wa kumtawadha huyu mgombea

Ninaomba kila siku Katiba mpya iruhusu urai pacha. Kwani soon Tanzania AMANI itatoweka!

Watanzania watawachoka hawa mabwanyenye na mabepali. Kisha watasema imetosha!
 
Mtu akifika mahali akaita mwanaye havintishi ujue huyo mtu ni kama kuku aliyekatwa kichwa
 
Vilaza wa Bavicha ni mzigo sana badala kujadili Chadema mtamsimamisha mgombea gani mnapoteza muda wenu kumjadili Ridhiwani hii ni dalili tosha ya kukata tamaa
 
Vikao halali vya chama au taasisi yoyote haviendeshwi kwa kuzingatia majungu au hisia bali kwa kufuata kanuni na sheria rasmi zinazojulikana!
Kama kuna mwenye uthibitisho kwamba Ridhiwani amefanya kosa lolote la kijinai au kimaadili apeleke pingamizi kwenye chama akiwa na ushahidi rasmi, vinginevyo itakuwa kama kelele za chura ambazo hazimzuii tembo kunywa maji.
Hata hivyo, pamoja na kwamba ni haki yake ya msingi na kikatiba kugombea uongozi, siyo vema sana kwa uongozi kulimbikizwa kwa baadhi tu ya familia, koo au kikundi fulani. Tunataka kuwepo social mobility kwenye jamii yetu yenye masikini wengi, watu wa lower class wapande middle na wa middle waende upper and vice versa. Hii inawezekana tu kama familia za juu hazitajilimbikizia hatamu za uongozi na mali.
Ni muhimu tujue kwamba hili siyo tatizo la Ridhiwani au baba yake Mh. J. Kikwete, Rais wa JMT, bali tatizo la mfumo mzima na halitamalizwa kutoa tuhuma zisizo na uthibitisho au majungu!
 
rizwani ana pesa kushinda wachaga wote kwa pamoja .safi sana riz mwanaume pesa shikamoo kelele tu

hivi kweli eeh? kazirithi kwa mrisho jakaya kikwete au na yeye ni jambazi kama wanavyowasema wachaga!?
 
Vilaza wa Bavicha ni mzigo sana badala kujadili Chadema mtamsimamisha mgombea gani mnapoteza muda wenu kumjadili Ridhiwani hii ni dalili tosha ya kukata tamaa

rais kikwete alikacha mdahalo na dr slaa kwenye uchaguzi wa 2010 je ridhiwani kikwete ataweza kupambana kwenye mdahalo wa uchaguzi wa ubunge au na yeye atakacha kama baba yake?
 
Back
Top Bottom