Rushwa iliyomwagwa kwenye kura za maoni za ubunge CCM Kyela inatisha, kuna mgombea amegawa pikipiki kwa kila katibu kata

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,599
217,991
Taarifa ya rushwa kwenye kura za maoni kwenye ubunge wa CCM Kyela kila mwananchi wa Kyela nikiwemo mimi anajua

Yuko mgombea mmoja ambaye alimwaga pikipiki kwa kila katibu wa kata kwenye jimbo hilo, kwa kadri ya ufahamu wangu kuhusu rushwa za uchaguzi wa ccm kyela, hii ni funga kazi, katika chaguzi zote nilizoshuhudia rushwa (maana ccm kila uchaguzi kuna rushwa ) rushwa hii ni kiboko! ujanja pekee aliofanya mgombea huyu ni kuanza mchakato wa rushwa kitambo, yeye hakutaka kusubiri wiki chache kabla ya kura za maoni, alianza kitambo kama yule wa Mbeya Mjini, pamoja na pikipiki siku chache kabla ya kura za maoni aliwamwagia wajumbe hadi laki 3 kwa kila mmoja kulingana na hadhi , swali ambalo wengi wamejiuliza ni kule alikotoa hela hizo.

Bali duru za waona mbali zimenasa chanzo chake cha mapato kilitokana na wale walioumizwa na kashfa ya Richmond akiwemo mmoja anayeitwa King maker, ambaye alijiapiza kwamba mbunge aliyekuwepo hatoboi, na hivi ninavyoandika hili kuna wapambe 18 wanahojiwa na TAKUKURU Kyela kwa kunaswa wakigawa hela kama mchanga , japo juhudi za kuficha jambo hili zinaendelea.

Mgombea mwingine aliyemwaga rushwa anatajwa kuwa diwani wa baraza lililopita ambaye amepata pesa kutoka kwenye makampuni yaliyokuwa yananunua cocoa, hasa baada ya makampuni hayo kuumizwa na utaratibu mpya wa wakulima kuuza cocoa kwenye chama cha ushirika, jambo lililosababisha makampuni hayo kukosa cocoa, mgombea huyo ameahidi akipitishwa atarejesha utaratibu wa zamani wa makampuni hayo kununua cocoa na kufuta chama cha ushirika, hela aliyomwaga haiendani kabisa na kipato chake .

Kwa ujumla Kyela wagombea wote walimwaga rushwa lakini kiwango kilizidiana, hii inahitimisha kauli za wengi kwamba bila rushwa si rahisi wajumbe kukuelewa

Tutaendelea kukuletea habari za uchaguzi na makandokando yake kwenye jimbo la Kyela bila kukupunja .

...Itaendelea .....
 
Back
Top Bottom