Naombeni ushauri

Naombeni ushauri

Mabawe

Member
Joined
Jun 22, 2014
Posts
22
Reaction score
0
Habarini za kazi,

Kuna kijana nilikutana nae mwaka 2011, tukawa marafiki hatimae apenzi mpaka wazazi wake wakafahamu na baadhi ya ndugu zake, mwaka 2011 december alisafiri kwenda nje ya nchi a wakati huo tulikuwa tukiwasiliana bila matatizo.Huku nyuma kuna mdogo wake wa kike ameolewa lakini amejengewa nyumba karibu na kwao, ila wakati huo mumewe hakuwepo, nakumbuka ilikuwa siku ya alhamisi aliniomba nimpe kampani tutoke usiku nikamwambia mie sitaweza kwasababu kesho yake nilikuwa naenda kazini na yeye hakuwa na kazi ni mama wa nyumbani, akaniambia anajisikiakutoka nikamwambia kama ni hivyo basi jmoc nitatoka na rafiki yangu kama unaweza twende hakunijibu lakini nilipomwambia rafiki yangu akaniambia kuwa makini na mawafi na hatukwenda nae. ilipofika January katikati kaka mtu ambae ndo mpenzi wangu alirudi, mie sina hili wala lile kumbe wifi yangu amemwabia kaka yake kuwa mie ni malaya naenda kujiuza usiku, kaka mtu akanijia juu akanitukana matusi mengi ya nguoni akaniambia hanitaki tena, nikaona isiwe tabu nikakata mawasiliano nikaendelea na maisha yangu,baada ya kama wiki mpenzi wangu aliniita tukayamaliza na akaniambia kuwa dada yak ndio alimwambia nikayachukulia kawaida sikumuuliza maisha yakaendelea, mie nilikuwa nimepanga chumba karibu na kwao mpenzi wangu na yeye badae akahama akahamia mwembechai nikamsaidia kununua baadhi ya vitu akaanza maisha na mie wakati mwingine nilikuwa naenda nakaa kwake wiki then narudi kwangu, kwa upande wake alikuwa haji kulala kwangu kwasababu nilikuwa naishi karibu na kwao na nyumba niliyokuwa nimepanga walikuwa hawana maelewano mazuri, ila kuna siku alikuja kulala kwangu bila taarifa lakini nikaona haina shida kwakuwa ni mpenzi wangu kumbe alikuwa na yake imefika saa tano za usiku simu yangu ikaita namba ilikuwa ngeni yeye kusikia imeita akanilazimisha weka loudspeaker kwakuwa nilikuwa najiamini nikaweka nikamuuliza nani mwenzangu akasema anaitwa luquman nikamuuliza wa wapi mbona sikufahamu na namba hii wewe umeitoa wapi akasema wewe si mabawe namba umenipa mwenyewe nikamwambia mbona sikukumbuki nilivyoanza kumbana akakata simu tukaanza kugombana na mpenzi wangu nikamwambia mie simjui kama kawaida alinitukana matusi ya nguoni, baada ya hapo nikaamua kukata mawasiliano na nikaondoka kwangu kwa muda akawa hajui niko wapi baada ya siku 2 alinipigia sikupokea karibu wiki mbili akaanza kunibembeleza turudiane kwakuwa nampenda tukarudiana na akataka tukaishi wote,nikakubali lakini chumba changu sikukiachia mwaka 2012 march nikangundua ni mjamzito nilisita kumwambia kutokana na tabia yake baadae akagundua akaniuliza nikamwambia ndio akaonyesha amekubali nilifikisha miezi 4 matatizo yakaanza akadai mimba si yake hawezi nihudumia mpaka nijifungue sikupata msaada wowote mpaka nimejifungua na nilipata matatizo nikajifungua kwa operation baada ya kujifunga nakurud nyumbani baba mtoto alikuja na dada yake wakawwameleta nguo katika maongenzi baba mtoto akaanza kutukana wakanyanyuka na kuodoka tangu hapo haleti matumizi baada ya miezi miwili nikarudi kazini kazi ambayo alinitafutia kampuni binfsi lakini sikuwa na cheti nilifanya kwa uzoefu lakini ikawa nafanya kazi kwa ajili yake akitaka pesa ananiomba hakuwa na kazi, siku niliyoriport kazini niliomba niwenawahi kunyonyesha nikakataliwa na matusi nikaamua kuacha kazi wakati huo mama yangu ndo aliekua ananihudumia baba mtoto alipoujua kazi sina akaanza kunikashifu kuwa sitopata kazi kama hiyo na hata nikipata mshahara hautafikia pale ila nashukuru mungu nipata kazi nzuri na amerudisha maelewano ila tatizo nikimwambia matumizi ya mtoto ananitukana na hatoi na kule nimehama na hapajui nilipohamia juzi jpili alitaka nimwelekeze madai anakuja kumuona mtoto nimekataa amenitumia sms za matusi siwezi hata yatamka na sitaki apajue ninapoishi.Nimechanganyikwa naombeni ushauri na samahanini kwa kuwachosha kwa urefu wa habari.
 
Sasa unaomba ushauri gani?…ww km hutak tena kuwa nae kata mawasiliano kbs atakupotezea muda
 
Fupisha. Kuna maneno 549 hapo. Maneno 100 yanatosha kufikisha ujumbe huo huo
 
kweli umechanganyikiwa... una penzi la dhati kwa jamaa ila jamaa hajitambui ndo maana unachanganyikiwa.....watu wanapata wasichana wema wao wanawachezea, siku akipata hawa wasumbufu atakoma.
 
Mmh...pole sana...huyo jamaa nae mbona anapenda kutukana Hivyo?
 
asante nimejaribu kuongea nae angalau basi asikane lakini ndo hivyo haelewi[/QUOTE]
Huyo mpotezee hana maana kabisa
 
Achana naye Huyo mtu kwa Muda kuwa peke yako kwanza mpaka atambue nafasi yako kama no wako niwako tu
 
Achana naye Huyo mtu kwa Muda kuwa peke yako kwanza mpaka atambue nafasi yako kama no wako niwako tu
Kwamba kuna siku atajitambua, siku hiyo haipo. Amini nakwambia haitakuwepo. Akiamua kuolewa naye ajue ndio itakuwa balaa kuliko anavyosimulia sasa. Wakina dada huwa nawashangaa sana, MUNGu anakuinesha uhalisia wa tabia ya mtu, lakini hutaki kukubali eti kwa sababu unampenda sana. Hakuna kitu kama hicho. Akumbuke kuna siku mapenzi yataisha atarudhi hapa hapa jamvini kuomba ushauri. Afanye uamuzi sasa, the sooner the better. HUyo ni majanga
 
ish!
si ulee mwanao mwenyewe?
Hapo ndipo ninapowashangaa wanawake wa bongo, ten kaeleza yeye ndio anafanya kazi, na huyo bwana mkubwa kazi yake kuomba pesa kwake, na matusi juu. Nadhani huyu dada mwenye uzi ndio majanga
 
Achana naye Huyo mtu kwa Muda kuwa peke yako kwanza mpaka atambue nafasi yako kama no wako niwako tu
Sio waachane kwa muda, halafu iweje? Kwamba atabadilika? Hakuna kitu kama hicho. Yeye aamue kuwa naye ili ataabike for life, au aangalie maisha upande mwingine
 
Back
Top Bottom