Nafikiri jibu umetoa mwenyewe, unahisi si chaguo lako. Kama ni hivyo, fanya maamuzi magumu, jifunge kiume mweleze ukweli na songa mbele ukiyasahau yaliyopita, na kuyachuchumilia yaliyo mbele yako. Na uwahi kufanya maamuzi mapema kabla hajakutega na mimba ukakwama kabisa kufikia malengo yako.