Nyoka kibisa
JF-Expert Member
- Nov 30, 2014
- 947
- 2,601
Mimi ni mwalimu lakini kipindi nikiwa o-level moja ya ndoto zangu ilikuwa ni kusomea pharmacy ili nije nifungue duka langu la madawa muhimu na kuuza mwenyewe lakni ilibidi nibadili baada ya kusimamisha bendera katika somo la kemia (chemistry) baadae nkaendelea na kozi ya ualimu ila baada ya kukaa kwa muda bado mawazo yangu yalikuwepo kwenye maswala ya u pharmac hivo nikaja na wazo mbadala kuanzisha duka la dawa (dawa muhimu) na nikaanza kujipanga panga mpaka sasa nina akiba ya kama 2.3ml kama mtaji lakini baada ya kuwashirikisha wadau wawili watatu wamenipa ushauri kuwa ni bora hicho kiasi nikitumie kwa ajili ya kurisit ili niwe na sifa za kuniwezesha kusomea u pharmacy ngazi ya cheti pia wengine wamenishauri nifungue tu duka alafu nitafute mtaalamu asimamie.
Naombeni ushauri kwa maana kila nikisikia mawazo ya wadau hata ile hali ya uthubutu niliokuwa nataka kuwa nayo inafifia kabisa na je kwa wale wazoefu wa mambo ya kuuza madawa hicho kiasi nilichonacho kinatosha kama kianzio huku naongezea kidogo kidogo au nitumie njia gani ambayo inaweza kuwa sahihi zaidi kufikia malengo yangu.