Pole sana mama D, ila nahisi huyo mwanaume anapata hela ya kutosha ila sababu inagawanywa familia mbili tofauti na ndio maana inaonekana haitoshi.
Mwambie dadako asitishe misaada kwenye familia ya huyo mwanaume na ajijenge kimaisha vizuri, pia ahakikishe watoto wake wanasoma vizuri bila ya shida.
Haina haja ya kuongea tena na mumewe kuhusu hilo jambo kwani amesalitiwa muda mrefu sana na amejiona ni haki yake kuendelea kumsaliti dadako.
Mwisho aanze maisha kivyake yaani aachane na huyo mwanaume kwani siku hizi magonjwa ni mengi sana.