Naombeni ushauri wanajamii...

Eamon Jacky

New Member
Feb 7, 2017
4
2
Nina mpenzi, huu ni mwaka wa pili sasa tupo kwenye mahusiano. Ila kwa bahati mbaya au nzuri, hatuishi pamoja kwa sasa mimi nipo Manyara kikazi na yeye yupo Songea kikazi. Kuna ugomvi ulitokea kati yetu hivi karibuni, alinikuta nawasiliana na ex wangu japo kuwa yalikua ni mazungumzo ya kawaida tu na wala hatukua na lengo baya ni basi tu kujuliana hali.

Ila kilichomkasirisha yeye sio kuwasiliana nae bali ni kukuta ile namba ya ex wangu kwemye simu yangu tena na tunawasaliana wakati yeye mwenyewe ndio aliifutaga kwenye simu yangu kipindi cha nyuma. Ameniblock kila sehemu mpaka instagram ameniunfollow leo ni siku ya nne.

Bado nampenda sana na nina malengo nae. Naombeni ushauri, nifanyaje?
 
Nina mpenzi,huu ni mwaka wa pili sasa tupo kwenye mahusiano.Ila kwa bahati mbaya au nzuri,hatuishi pamoja kwasasa mimi nipo Manyara kikazi na yeye yupo Songea kikazi.Kuna ugomvi ulitokea kati yetu hivi karibuni,alinikuta nawasiliana na ex
Kuna demu nimelala nae hapa anakata simu kila dakika, then naona kabloku namba alafu naona anambloku mtu Instagram, Facebook, Twitter, WhatsApp, sijui huyo jamaa kamuuzi nini hapa songea.
 
Usiseme unampenda sana, ungempenda usingemfanya fala. Kafuta Namba we umeitafuta na umeendelea kuwasiliana nae. Wewe ni lofa

Usijifanye kumpenda, we unampenda ex wako ambae hakupendi ndio maana alikuacha.

Ujinga zaidi ni kusema mnawasiliana mambo ya kawaida
 
Hata ningekua mimi ningekasirika na inaonekana bado unampenda Ex wako ndio sababu hukomi kuwasiliana nae. Mimi sina hata ushauri nikupe tu pole.
 
Tufanye icho ulichokifanya angekifanye yeye alafu akakwambia ni mazungumzo ya kawaida tu ungekubali?
Mshika mbili moja umponyoka nenda kwa ex kajipoze machungu
Maex wakishaona Mambo yako yanaenda kuwa mazuri wanageukaga wachawi
Au siyo? Kikulacho ki nguoni mwako
 
Usiseme unampenda sana, ungempenda usingemfanya fala. Kafuta Namba we umeitafuta na umeendelea kuwasiliana nae. Wewe ni lofa

Usijifanye kumpenda, we unampenda ex wako ambae hakupendi ndio maana alikuacha.

Ujinga zaidi ni kusema mnawasiliana mambo ya kawaida
Sasa hapa ushauri ni nini jomoni? Mtumie angalau dola 100 akampoze basi. haha (joking!)
 
Ndio maana hata huyo x wako alikuacha ......akili yako ni sifuri ..
Am sorry
 
Nina mpenzi,huu ni mwaka wa pili sasa tupo kwenye mahusiano.Ila kwa bahati mbaya au nzuri,hatuishi pamoja kwasasa mimi nipo Manyara kikazi na yeye yupo Songea kikazi.Kuna ugomvi ulitokea kati yetu hivi karibuni,alinikuta nawasiliana na ex wangu japo kuwa yalikua ni mazungumzo ya kawaida tu na wala hatukua na lengo baya ni basi tu kujuliana hali.Ila kilichomkasirisha yeye sio kuwasiliana nae bali ni kukuta ile namba ya ex wangu kwemye simu yangu tena na tunawasaliana wakati yeye mwenyewe ndio aliifutaga kwenye simu yangu kipindi cha nyuma.Ameniblock kila sehemu mpaka instagram ameniunfollow leo ni siku ya nne.Bado nampenda sana na nina malengo nae.Naombeni ushauri,nifanyaje?
Huna akili
 
Sio kila mtu ana uwezo wa kupend kwa hiyo nakupa hongera sana. Humu ndani JF kuna marobot na watakupiga majungu kweli kweli kana kwamba wao hawalilii mapenzi. Kikubwa ukiwa na mpenzi wako jitahidi ufahamiane na marafiki au ndugu zake wa karibu vitu kama hivi sio vya kuomba ushauri. .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom