Naombeni ushauri uvimbe huu unanitesa

Naombeni ushauri uvimbe huu unanitesa

DREAMBOY

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Posts
2,117
Reaction score
1,372
Naombeni ushauri au tiba.

Mimi nasumbuliwa na tatizo la uvimbe chini ya tako la kushoto katikati ya korodani na njia ya haja kubwa!

Tatizo lilianza kutokana na kupata choo ngumu, hivyo kila ninapopata choo inayohitaji kusukuma kuna kijiuvimbe hushuka pembeni ya njia ya haja kubwa na kina maumivu fulani, na ikishatokea hiyo hali maumivu yanaweza kudumu hata baada ya siku nne ukikaa unasikia tu.

Na uvimbe ukipapasa unausikia. Jambo linalonistua ni kuwa limekuwa likitokea mara kwa mara.

Ombi: Ushauri, ama uzoefu kwa aliwahi kukutwa na tatizo hili au dawa za kienyeji au hospitalini.

Angalizo: Watu wengine wananiambia sio wa hospitalini, japo sijawaamini. Nipo njia panda!
 
ukiwah linatibika otherwise utafanyiwa upasuaji mdogo kuondoa uvimbe
Hakuna uvimbe kwa kuoneka yaani kama mwinuko fulani. Pia dokta vp dawa zake ni zpi na vpimo vyake vikoje
 
Hospital hata ya levo ya kituo cha afya inatibu? Au mpaka hospital ya Mkoa ,nasema hivyo kwa sababu nipo mbali na mjini
Tatizo hilo sio kubwa. Nenda kituo chochote cha afya utapewa maelekezo dawa gani utumie kulingana na ukubwa wa tatizo, kama hawana watakuandikai utatafuta kwenye famasi Yoyote.

Ukichelewa uvimbe utakuwa mkubwa. Ukipasuka itabidi upasuaji.

Pia punguza kula nyama mkuu mmeng,enyo wake unachukua muda tumboni, kula mboga mboga ,matunda,punguza Wanga.

Usisahau na jwisi ya ukwaju inasaidia sana kumengenya chakula kwa haraka zaidi ,pia kunywa maji mengi uwezavyo.

Kufanya hivyo kutapunguza muda wa kukaa chooni. Kumbuka unavyotumia muda mwingi na pressure kubwa ndio tatizo linazidi kuwa kubwa.

Hospital wanatoa dawa unaweza pona kabisa, lakini usipofata utaratibu huo hapo juu tatizo linaweza kujirudia tena.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna uvimbe kwa kuoneka yaani kama mwinuko fulani. Pia dokta vp dawa zake ni zpi na vpimo vyake vikoje
kuna dawa ukienda hospital utapewa Kuna za kuingiza sehemu ya haja kubwa pia na vidonge unameza na utapewa dawa ya kupaka sehemu hiyo ya haja kubwa
 
Sijui unafanya nini hapa mkuu fanya uwahi hospital ukapate matibabu sahihi na kuna hizi dawa za kienyeji wanatangaza mtaani kwamba zinatibu bawasiri haishauriwi kutumia dawa kabla hujakutana na wataalamu wa afya wakakupa vielelezo hasa maradhi yako yapo ktk stage gani kama ufanyiwe upasuaji au upewe dawa,muuza dawa za kienyeji hana idea ya kujua tatizo limefikia hatua gani sababu hafanyi uchunguzi wowote.

Jamaa yangu Bon tulimzika pale makaburi ya Mburahati mwaka 2017 kwa ugonjwa huu baada ya kuwa anafanya siri huku akitumia madawa ya kienyeji siku hali imebadilika ghafla kupelekwa hosp wakashauri upasuaji wakakuta imeshaathiri mpaka utumbo mkubwa,mwamba aliondoka kama masihara mchana wa saa 7.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Mkuu hiyo ni bawasiri ila inatibika iwahi kuna vidonge wanaweza kukupa unaingiza kwenye kinyeleo(ndukum) kwa muda inapona,kula mlo sahihi mkuu,maji mengi ila usibebe vitu vizito pia sana ila kama uko kwenye sekta ya ulinzi huo ugonjwa upo sana kulingana na majukumu ya kule hasa kipindi cha kozi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mtu kanitisha kwel, eti ukifanyiwa opereshen huponi et tatizo linatibiwa kiinyeji
 
Kuna mtu kanitisha kwel, eti ukifanyiwa opereshen huponi et tatizo linatibiwa kiinyeji
Sir_Mimi,
Bro . Unanitisha ile mbaya
Usije kuwa unachanganya nilichokiandika post #15,nilichosema usirubuniwe na watu wanaouza madawa ya kienyeji kutumia dawa zao bila kujua tatizo lako limefikia stage gani nenda kwenye matibabu ya kisasa utapona,obviously ugonjwa wowote ukiuzembea utakuuwa so usiseme nimekutisha wahi hospital.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
pole sana mwana..kwahiyo ww kukata gogo ni kama upo vitani...

tembelea wataalamu wa afya watakushauri vema..

Jf Doctors wapo humu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom