Naombeni ushauri tafadhari

Naombeni ushauri tafadhari

The Senetor

Member
Joined
Aug 23, 2014
Posts
41
Reaction score
23
Wakuu poleni kwa majukumu, mimi si mwenyeji sana humu ila ndugu yenu nina jambo linanitatiza sana. Niliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na binti mmoja ambaye nilidumu nae kwa miaka 3 nilimsaidia hadi akafika chuo kikuu na nilipotaka kumwoa familia yake waliomba nimsubiri amalize masomo basi nilichofanya niliamua kumvisha pete ya uchumba kuonyesha upendo wangu kwake.

Baadae alibadilika sana na nikaja gundua ananisaliti kwa kuwa na uhusiano na mwanaume mwingine kwa muda wa mwaka mmoja.Niliumia sana na nikajitoa kwenye msururu baadae waliachana na jamaa na mimi baada ya miezi 6 nikatafuta mwanamke mwingine, julai mwaka huu akaanza kunitafuta kwa bidii nilimzuia asinipigie wala kunitumia sms lengo likiwa ni kumsahau kirahisi.

Huyu niliyenae ni mwelewa,ananiheshimu sana na kunipenda sana pia kimapenzi anajiweza mno yaani sijawahi kupata mwanamke anayenipa utamu kama yeye na sasa hivi ana mimba yangu ya miezi minne. Tatizo nililonalo ni mimi kumkumbuka sana yule ex kiasi natamani kumpigia simu na bado nampenda sana kweli moyo wangu unanirudisha sana nyuma nimejaribu kumsahau ili nimpende huyu lakini muda mwingi namwaza yule mwingine.

Wakuu samahani sana kama nitawakera nishaurini nifanyeje ili nimsahau na nimpende shemeji/wifi yenu mwenye mimba yangu au niwe nawasiliana nae kama rafiki tu.Samahanini sana kwa maneno mengi..
 
Wakuu poleni kwa majukumu,mimi si mwenyeji sana humu ila ndugu yenu nina jambo linanitatiza sana.Niliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na binti mmoja ambaye nilidumu nae kwa miaka 3 nilimsaidia hadi akafika chuo kikuu na nilipotaka kumwoa familia yake waliomba nimsubiri amalize masomo basi nilichofanya niliamua kumvisha pete ya uchumba kuonyesha upendo wangu kwake.Baadae alibadilika sana na nikaja gundua ananisaliti kwa kuwa na uhusiano na mwanaume mwingine kwa muda wa mwaka mmoja.Niliumia sana na nikajitoa kwenye msururu baadae waliachana na jamaa na mimi baada ya miezi 6 nikatafuta mwanamke mwingine,julai mwaka huu akaanza kunitafuta kwa bidii nilimzuia asinipigie wala kunitumia sms lengo likiwa ni kumsahau kirahisi.Huyu niliyenae ni mwelewa,ananiheshimu sana na kunipenda sana pia kimapenzi anajiweza mno yaani sijawahi kupata mwanamke anayenipa utamu kama yeye na sasa hivi ana mimba yangu ya miezi minne.Tatizo nililonalo ni mimi kumkumbuka sana yule ex kiasi natamani kumpigia simu na bado nampenda sana kweli moyo wangu unanirudisha sana nyuma nimejaribu kumsahau ili nimpende huyu lakini muda mwingi namwaza yule mwingine wakuu samahani sana kama nitawakera nishaurini nifanyeje ili nimsahau na nimpende shemeji/wifi yenu mwenye mimba yangu au niwe nawasiliana nae kama rafiki tu.Samahanini sana kwa maneno mengi..

Acha uzoba wewe,utampendaje mtu akupendi na utamsomeshaje mtu kwa ambae sio ndugu yako.Tembea na wanawake mia mbili ndipo uowe.
 
Ndani kabisa Kuna maamuzi umeshafanya na huyapendi yanakuumiza unafuta namna ya kuyahalalisha kupitia maoni mbalimblai yenye mtizamo huo ila kwa yote utayofanya just watch the time coz there is no way u can bring it back.
 
Unatafuta janga.....

Wanasema mkataa pepa pabaya panamuita

Na wewe panaya panakuita
 
wadogo zako kijijini wanakosa elimu, wewe unasomesha mtu mliokutana nae ukubwani. kwa habari yako hii ukitaka kumsahau kila siku kunywa viroba. maana moyo wako haujielewi.
 
Unauhakika gani kama hiyo mimba ni yako? Wewe hukuwahi kumsaliti huyo demu wako wa kwanza kabla ya kugundua unasalitiwa? Huyo uliyom-mimba ulimkuta na bikira? Kama hakuwa na bikira basi na yeye anawawazia wanaume wengine waliyompitia kabla yako. Ukitaka ndoa/ mahusiano ya kweli kuwa tayari kusamehe na kusahau bila kujali ukubwa wa kosa na ujifunze kuishi na tofauti na mapungufu ya mwenza wako.
Mwanaume inatakiwa usumbuliwe na PESA na siyo mapenzi au mwanamke, pia usimchunge mwanamke, zichunge PESA, wanawake ni wengi hata wa kuokota wapo, PESA utaziokotea wapi?
 
unataka kutumia akili zetu badala ya zako?
 
UMenisononesha sana ndugu. Usije kumtenda vibaya uyo anayekupenda kwa dhati.
Pia mwenye akili timamu hawezi kurudia matapishi.Kuna wakati tunatakiwa tukutane na mabaya ili tunapopata mazuri tujue thamani yake.
 
Huwezi kuwasiliana na mtu wako wa zamani bila kukumbushia. Hakuna urafiki wa namna hiyo. Tena umesema unampenda. Hapo ndo huwezi kabisa kuzuia dhambi kutendeka
 
huyu ulimpa mimba yanini kama bado ulikua unamkumbuka yuleeee???????? acha upoyoyo ushamharibia huyu maisha umwachie nani??????? wew unamkumbka yey hakufikirii hata sekunde ndomana akakuacha........tulia na uliyenae....
 
Hivi unafikir maneno yetu yataurudisha moyo wako??

Kama umeshindwa kukumbuka maumivu aliyokupa na umeamua kuyafuta mabaya aliyokufanyia na umeyasafisha yamekuwa meupe kama theruji sisi ni akina nani hasa mpaka tuyatie doa tena ili uanze kumchukia au kumsahau?

Huwa nasikitika sana pale mtu hasa mwanaume anapopata pumziko lakn anakuwa kipofu gafla na kukimbilia jangwan...

Kweli unaweza kuona na usijue na unaweza kusikia na usielewe.
............................................ ...........................
 
mambo mengine inatakiwa uyasolve mwenyewe kwa sababu anayejua uzuri na ubaya wa hao wanawake ni wewe na atakayeishi na yeyote kati yao ni wewe mwenyewe asa tukushauri sie tutayawezea wapi na ushasema huyo wa sasa anakupa penzi hujawahi kutana nalo pagumu hapo. follow your heart
 
Umesahau nini kwa huyo demu wako wa zamani? Kuna kipi ambacho ndo unafikiri umekumusi sana kutoka kwake.
Ushauri wangu anza kumpigia simu huyo demu wako wa zamani, panga naye ahadi uonane naye,na ikiwezekana endelea kuwasiliana na kukutana angalau mara 1 kwa wiki. Ila kumbuka kufanya hivi kwa siri kubwa bila yule mwenyw mimba kujua.

Endelea kuwasiliana naye tu na kufanya yenu jadi hapo utakapoona inatosha utaacha tu. Kuacha huwa kuna kuja automatic. Siyo kitu cha kulazimisha. Kama unaona haiji automatic basi endelea naye tu. Ikiwezekana huyu naye mpe mimba.
 
Kwanza nauliza hivi
Huyu mwenye mimba umemuoa?
Au mpo tu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom