Naombeni ushauri nipo njia panda

Habarini wana JF,

Kwanza niwatakie heri ya sikukuu ya wapendanao mzidi kupendana. Tukirudi katika mada mimi ni mwanamke wa miaka 25 na mama wa mtoto mmoja. Nina mwenza wangu ambae ndio baba wa mtoto wangu.
Kinachonifanya niombe ushauri ni hali iliyopo sasa.
Mwaka jana mwezi wa 6 mwenzi wangu alikuja kutoa mahari kwetu na kunivalisha pete ya uchumba wakati huo nilikuwa na mimba ya miezi 5.

Upande wa kiume wakaahidi tufunge ndoa mwezi wa 12 lakini ikaonekana kama Mungu akijalia nitajifungua salama basi mtoto atakuwa mdogo sana basi wakasogeza mpaka mwezi wa 4 mwaka huu na wakasema inabidi nikajifungue kwa mamamkwe na nitakuwa chini ya uangalizi wake .
namshukuru Mungu nilijifungua salama.

Sasa hivi mtoto ana miezi 5 wazazi wangu wanasema nirudi nyumbani sababu sijaolewa mpaka wanikabidhi kwa ndoa kabisa ila mama mkwe anasema nibaki sababu mahari ni ndoa tayari kanisani kubariki tuu mimi ni mke wa mtu. mchumba wangu ananiambia nikiondoka kurudi kwetu niondoke moja kwa moja nisirudi kwake. naombeni ushauri wenu juu ya hili.
Je ni kweli ukishatolewa mahari unakuwa umeolewa? Na nifanye nini katika hili? Mimi ni mbena na mchumba wangu ni mchaga.
Natanguliza shukrani.

Sent using Jamii Forums mobile app
The same case to me ,na kwa sasa tumetengana ,wazazi wake walumwambia arudi kwao alirudi ,na sasa hatupo pamoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mimi imani yangu bado sijawa yaani hata sielewi...nao walisema tunamuazima kwa kipindi ambacho atajifungua awe chini ya mama mkwe

Sent using Jamii Forums mobile app
Na hilo linaonekana wamekosea toka mwanzo walipo mruhusu kwenda kujifungulia huko kwa mkwe,sasa wanataka wasawazishe kosa maana watu wengine wamezoea kuoa uzeeni.ushauri kwa hiyo mke wazazi wako wanataka ndoa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni dini gani??

Kama n muslim ndoa ina nguzo zake, lazima mawalii wa pande zote mbili wawepo na watoe idhini ya kukuozesha kama hili halijapita wewe bado kua mke

Hata kama anataka kukuoa lakini lazima aheshim mawazo ya wazazi wako, imagine umezaliwa wazazi wako wakateseka kukulea kwa shida na raha ukawa hivi had nawe waenda itwa mama leo uwakaidi

Siamini sana kwenye ndoa za kimila, nimeshahudia pia watu wametolewa mahari harusi ikapangwa na bado ndoa haikua kiimani hujakua mke halali bado.

Ukitolewa mahari ww ni mchumba wa mtu sio mke.
 
Mimi ni mkristo...mkatoliki hata wazazi pia wamesema ukitolewa mahari kama hakutakuwa na ndoa karibuni kuna namna ambayo wazazi wanakuaga na kukukabidhi kwa mchumba wako lakinibwao walisema tuu tunamuazima ili ajifungue kwenye uangalizi wa mama mkwe. na kweli siwezi kukaidi wazazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiwakaidi wazazi wako, na mtoto kwa mama hakui sikiliza wazazi wako huyo hajawa mume rasmi bali mchumba tena mchumba halali sababu mahari tayari.
Mimi ni mkristo...mkatoliki hata wazazi pia wamesema ukitolewa mahari kama hakutakuwa na ndoa karibuni kuna namna ambayo wazazi wanakuaga na kukukabidhi kwa mchumba wako lakinibwao walisema tuu tunamuazima ili ajifungue kwenye uangalizi wa mama mkwe. na kweli siwezi kukaidi wazazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni mkristo...mkatoliki hata wazazi pia wamesema ukitolewa mahari kama hakutakuwa na ndoa karibuni kuna namna ambayo wazazi wanakuaga na kukukabidhi kwa mchumba wako lakinibwao walisema tuu tunamuazima ili ajifungue kwenye uangalizi wa mama mkwe. na kweli siwezi kukaidi wazazi

Sent using Jamii Forums mobile app
Basi huyo jamaa anataka ukosane na wazazi wako kwani walijua zima tu kwa makubaliano leo wanaouhitaji ili wafuate utaratibu ifuatwe wanakuzuia!jaribu kumkumbusha na ukiona hajielewi huyo sio muoaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom