Naombeni ushauri nataka niwe nawahi kuamka

Singida ndio home

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,188
3,360
Kwa muda mrefu sana nina tatizo la kuwahi kuamka asubuhi, Kwa kawaida hua naamka saa nne na nikiwahi basi ni saa mbili, Nawekaga alarm saa 11 asubuhi lakini hua naishia kuipuuza, sina mwajiri wa kuniwekea mashart niingir kazini saa ngapi, Nimejiajiri so hususan sekta ya kulimia watu mashamba kwa trekta nililokodisha so mimi hua naendaga kucheki progress ya vijana niliowaajiri huko shambani weekend maana ni mbali na ninapoishi hapa town...Naombeni ushauri wenu nitumie mbinuz zipi niwahi kuamka
 
Huwa unalala saa ngap? Jitahidi uwe unalala kabla ya saa nne ili uamke saa kumi na mbili, masaa nane kwa binadamu kulala ni yanatosha.
"Lakino" wewe una undugu na bambo?"
 
Ukiamua unaweza
Jiweke mazoea

Nilikuwa na mazoea ya kuamka saa 12 piga ua lazima mda huo ukifika nitakuwa macho

Ikafika kipindi mazoea ni kuamka saa 3 ,piga ua siwezi kuamka mapema mpaka saa 3

Niliweka mazoea nalala saa nane hili jambo lilinisumbua sana ,kila nikitaka kulala saa sita,saba au tano siwezi mpaka saa nane ndio usingizi huja

Kila jambo ni kuamua na mazoea ,ukiamua saa 11 uamke utaamka

Moyo ni kama mtoto mdogo ukimdekeza na kumzoesha ndivyo hivyo atakapodeka na kuzoea ,kama umeudekeza moyo na hujaamua haki ya mungu alarm utakuwa unazima kila siku

Konda analala saa 5/6 anaamka saa kumi

Amua ,jizoeshe ,ukishaamua kila siku mda huo utakuwa upo macho
 
Kama unatakiwa kuwaona wafanyakazi wako weekend tu basi siku zingine fuata your biological clock, lala utakapojisikia kulala, amka utakapojisikia kuamka. Kila mtu ana masaa yake ya ufanisi, jaribu kuangalia yako ni yepi na panga mipango yako mingi wakati huo.
 
Kwanza nakusifu sana kwa kujiajiri wakati wa weekend! Ningekushauri utafute shughuli nyingine weekdays ili uwe busy, maana an idol mind is a devil workshop!
 
Ni vizuri kujifahamu, either you are a night or morning person.
Pengine ni mtu wa usiku zaidi kwa hiyo unachelewa kulala na kuchelewa kuamka. Na kama ni hivi basi inakuwa ngumu kwako kulala mapema hata kama unapenda.
 
Back
Top Bottom