Naombeni ushauri kuhusu aina hii ya mwanamke

mkumbwa junior

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
805
1,541
Mwezi wa nne nikiwa safarini kutoa Arusha-Dar nilibahatika kukaa siti moja na Binti mrembo kweli kweli,,na alikuwa mchangamfu sana,tulioeana kwa muda mfupi tukapiga story nyingi sanaa sanaa,,tulivofika korogwe(hotelini) akaniomba simu yangu apige picha kadhaa sababu hakuwa ba smartphone kwa madai atakapofika dar akipta smartphone nitazimtumia,,sikuwa na hiyana akapiga picha nyingi n zingine tukapiga nae nikamlipia vitu alivyotumia hotelini tukarejea garini safari ikaendelea tukiwa kama mtu na mpenzi wake wa siku nyingi.

Bahati nzuri zaidi yule binti uelekeo wetu ulikuwa mmoja(tabata segerea) tulipofika ubungo alipokelewa na mwana mama mmoja ambae alinitambulisha ni mama yake mdogo,,mimi nilikuja pokelewa na kaka yangu ambae alikuka na usafiri binafsi kwa kuwa wao hawakuwa na usafiri ilibidi tuwachukue katika gari alilokuja nalo braza kunipokea, tukaondoka hadi wakafika wanapoishi sisi tukaendelea mbele kidogo,,hatukuwa tunaishi mbali sanaa,

TATIZO LIKAANZA

Baada ya kufika na kupumzika nikamtext binti sms hakujibu matokeo yake alinitumia please call me,,nikaamua kuonyesha uanaume nikamuunga kifurushi cha SMS cha siku 30 baada ya hapo nikapiga hakupokea,sms hakujibu,,hali ile ikaendelea kwa siku kama nne,,siku ya tano nikaenda kwao AJABU alinipokea kwa furaha sanaa akionyesha amenimiss na nikamuomba twende mahali hata tukapate kinywaji akakubali tukatoka nikamuuliza sana kwnini hapokei simu wala kujibu sms hakunipa jibu la maana,,ila akaniomba radhi kuwa tutakuwa tunawasiliana ajabu akaendeleaa vile vilee ila kila tunapokutana hata kwa bahati mbaua anakuwa mchangamfu sanaa siku moja nikaamua kubadilisha namba akapokea tukaongea kidogo sikujitambulisha nikakakata nikamtext kwa namba mpya akajibu,,nikamtext kwa yangu akakaa kimyaa.

Kuna siku usiku akanitext nimtumie picha zake nikatuma wasap ikaishia hapo nikimtext sms anasoma ila hajibu

Katika mambo ninayojikubali huwa ni kiwa na ulimi mlaini kwa mabiniti warembo,enzi nipo chuo baadhi ya marafiki zangu walifikia hatua ya kusema ninatumia dawa kuwanasa warembo kwani hakuna mtoto mzuri ambae ningemtaka akakataa hadi mimi mwenyewe sometime nilikuwa najishangaa na hadi leo bado nikitaka binti huwa ni ngumu kuchomoa japo sasa hivi nimepunguza sanaa kufungua fungua zipu hovyo ila kiukweli sijawahi kukutana na binti wa sampuli hii na naomba mabaharia wenzangu mnijuze mabinti kama hawa huwa zinatumika mbinu gani kuwanasaa
 
mi sinaga time ya kusumbuana na mwanamke hivyo!wao ndio huwa nawapa mda mwingi kunitafta!sina shobo ila akikaa na mi mda mchache tuu hatak hata kurud kwao
 
Huyo amekusoma amegundua ni mtu una maisha mazuri japo sio sana.

Kwa hiyo anataka utumie nguvu nyingi kumbembeleza ili akupige pesa.

Kuna baadhi ya wanawake ukimuonga kwa haraka au ukimpa ofa kwa haraka kabla hamjafahamiana vizuri wanatafsiri either wewe ni bwege au una pesa za mchezo.

Na ndio maana hata kama kimoyoni amekukubali tayari atakwepesha makusudi na kuigiza kama hakutaki ili akutumie atakavyo kukulia pesa.

Wazoefu wa mambo tumegundua hilo na kuna mbinu za kuepuka hayo na kumnasa siku za mbeleni.
 
Mkuu Mkuu hili niliwaza na moja ya mbinu niloamua kuja nayo ni kumpotezea kwa sasa hata tukikutana akinichangamkia namjibu vizuri then namwambia kuna mahali nawahi....
Vpi hii itanisaidia??
Huyo amekusoma amegundua ni mtu una maisha mazuri japo sio sana.
Kwa hiyo anataka utumie nguvu nyingi kumbembeleza ili akupige pesa.
Kuna baadhi ya wanawake ukimuonga kwa haraka au ukimpa ofa kwa haraka kabla hamjafahamiana vizuri wanatafsiri either wewe ni bwege au una pesa za mchezo.
Na ndio maana hata kama kimoyoni amekukubali tayari atakwepesha makusudi na kuigiza kama hakutaki ili akutumie atakavyo kukulia pesa.
Wazoefu wa mambo tumegundua hilo na kuna mbinu za kuepuka hayo na kumnasa siku za mbeleni.
 
Yes ndio hiyo mbinu nilitaka kukwambia.
Mpotezee na umfute kabisa kichwani na ikiwezekana upate mwanamke mwingine wa kukuliwaza.
Ukishamkazia hivyo yeye mwenyewe atakutafuta na kujirahisisha kisha unamaliza kazi.
Asipokutafuta basi ujue ana mtu mwingine ambaye ana future naye.
Mkuu Mkuu hili niliwaza na moja ya mbinu niloamua kuja nayo ni kumpotezea kwa sasa hata tukikutana akinichangamkia namjibu vizuri then namwambia kuna mahali nawahi....
Vpi hii itanisaidia??
 
Hakuna kitu kinanipa uvivu kama kuchat chat haswa text za kawaida ndio napata uvivu
Mie whatsap au calls zisizo na maana ndo siwez kbs! Nikikuheshim naijibi after hours!...khaa! Mtu anachat na ww anakiambia "niambie"hapo una mambo mob ya kufanya...hahahaa!
 
Watu awapendagi mameseji kibao /Mtu smart na makini ,,hawezi kukaa anamfukuzia demu kwa kumtumia mameseji kibao.
 
Uwe unamtumia hela kwenye simu yake badala ya kupoteza muda wako kumuunga hicho kifurushi cha sms.
 
Back
Top Bottom