DAFU NA NDIMU, Hili jambo linanitesa sana natamani saaana kuona wazazi wangu wakiishi pamoja mimi nimeshasamehe ila kwa upande wa mama ukiliongelea sana utashangaa anapanga safari ya ghafla kwenda nje. Hapo na mawasiliano yatakataa kwa muda.
Ebu chukulia nafasi ya baba ndo yako maana hata wewe mbeleni utakuja kuwa na familia kama baba yako. Mungu anasema samehe naye atakusamehe. Wanawake wengi ni wagumu wa kusamehe. Wao wanapenda kurundika makosa yote hata kama la mwaka 47 halisahau hivyo inakuwa ngumu kwake kuachia moyo maana ana rundo. Ushauri wangu wewe endelea tu na maisha wape wote upendo sawa. Ukiegemea kwa mama tu baba atajua unaunga mkono msimamo wa mama yako. Big up to your dady ameweza kuomba msamaha.