Naombeni ushauri juu ya familia yangu

Karimu123

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
243
114
Habari wanaJF nimeona nije kwenye hili jukwaaa mana najua hapa ntapata mawazo chanya.

Mim ni kijana 22yrs Old kwetu tulizaliwa wawil mimi na dada yangu alishaolewa ana maisha yake. Mimi kwa Bahati mbaya nilifeli form six hivyo niko tu nyumban toka mwaka 2015 ila nimejiajiri mwenyewe sema la ukweli kaz ninayofanya inanilipa kiasi kwamba ndani ya mwaka nimefanya vitu vikubwa kama kununua kiwanja takribani nusu heka maana mama yangu hakuweza kununua kiwanja na mzee wetu alitengana na mama baada ya kustaafu kazi na kurudi Moshi maana alioa mke wa ndoa.

Maisha ya Nyumbani ni magumu nisiseme uongo tuko kwenye ya kupanga mama yangu (Tuko wawili) alipata kazi miaka ya 2006 shule moja hapa mjini Arusha alilipwa vizuri lakini toka mwaka huo nyumban hakuna cha maana alicho kifanya hata makochi yenyewi ni majanga (ni mfujaji wa pesa) ukimleta mgeni yaani mpaka nasikiaga aibu inabidi nisepe kama juzi kuna mwanafunzi wake mmoja alikuja niliona aibu kiasi kwamba mama anajina kubwa huko nje lakini ukifika ndani kwake ni fedhea tupu ila ukimuliza hela zako unafanyia nini anakwambia nalipa kodi nimewasomesha wakati nimesoma serekalini toka vidudu mpaka kidato cha sita ada ni 200K kwa mwaka.

Baada ya kutolewa kazini amepata mafao yake mil 13M ametumia tumia zimebaki 10M cha ajabu ni kwamba mwaka jana nilimwambia nimepungukiwa na hela kidogo niongeze ninunue kiwanja akanipa kweli nikanunua kwa malengo ya kwamba akianza ujenzi nitamsaidia kidogo kidogo lakini sasa mambo yamebadilika kuna kipindi hapa katika nilikuwa broke vibaya ikabidi niombe hela sio nyingi angalau 100K ili niweze kurudi kwenye peak nisiguse hela kwenye mzunguko wa baseness

Basi lakini naona imefikia mahali nashindwa kumvumilia watu wakija anawaambia amenunua kiwanja cha 10M na bado ana mpango wa kuongeza tena nikiwa hapo mbele mimi si muongeaji sasa wengi kwa marafiki zake wanamuuliza huyu kijana wako anafanya nini hapa mbona hasomi anawaambia ataenda chuo mwakani sasa hiki kitu kina niumiza sana kuona kwamba hathamini mchango wangu nimejipinda kiasi gani lakini kuapriacite kuwa nimetafuta sehemu ya kukaa mbaya zaidi nina fikiria kurudi shule hasa mambo ya mifugo mana plan yang kubwa nije kuwa mfugaji lakin naona sielew itakuwaje uchumi wangu sio kwamba napenda pesa hapana ila naona nikiweka loose point kwenye biashara yang ni total loose haitachukua mwez nitafunga na muda wa kusoma mifugo ni kama miaka 3 samahan kwa essay ndefu roho yan inaniuma na sina mtu wa kushare nae matitzo naona huku ndo mahali sasa kwenu nataka kushauri vitu vifuatavyo

1. Je niende shule (Miaka 3) kabisa au nitafute short course za mifugo nisome hasa nguruwe na kuku wa mayai na nyama au niende shule kabisa.

2. Kutokana na mama yang amekuwa akinitawala kijinsia fulan je nifanye vitu vyangu kisir na vip niepuke hela zake mana naisi hiv viela ananipa ndo ananifanya mjinga hawezekan kitu cha sh 1000 ukajazia 100 alafu kikawa sote chetu simaanishi kwamba namnyima nilishwambia ajenge kwny hicho kiwanja mana anacash tayari mim najipanga taraitibu nitaanza tu.

Niombe radhi kwa post ndefu lakin sina jinsi naumia na sina mahal pa kusema zaid ya humu Asante nitapokea ushauri wenu kwa mikono miwli
 
Uyo ni bi mkubwa ako aliekuzaa au wa kufikia tu.
Sioni umuhim wa wew kuomba ushauri humu kwa suala kama hilo ulilolieza ukizingatia linamuhus mtu aliekuleta dunian.
Ndugu unasemaje viela vyake,kwanza jirekebishe kidog ni afadhali utafute siluhu mwenyew mambo ya mama usibe ushairi kwa watu wengine,uyo ni mama ako watu wengine wanamuona mwanamke wa kawaida tu.
Nakushauri usiombe ushaur jinsi ya kutatua tatizo na mama ako wee tafuta namna ya kufanya na si kumjwaza b mkubwa ako.
 
Kaa nae Ongea vizuri atakuelewa ndugu yangu.
Muulize pesa zake anapeleka wapi?
Mpe Tahadhari kuhusu kesho.
Mwambie atumie hela kwa vitu sahihi na vya maendeleo .
 
Biblia Inasema..

Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie. Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku............ Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi. Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku.Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu.............
 
Umejiajiri na inakulipa......

Unenunua nusu ekari....

Mmepanga, ndani kwenu aibu...mama yako hakuna lichofanya......... shame on you.... aibu yako kwa kuona aibu na kwenu..... kama unajua hakuna cha maana lichofanya mama yako kwa njji hayo makochi usinunue wewe?

Unasema hela amefanyia nini? Unadharau laki 200 ya ada? Unajua amejinyima mangapi ili kupata hiyo laki mbili????? Na baada ya kulipa laki 2 shule ndio basi? Hukusoma tuition, hukula chakula, hukununuliwa vitabu material photocopy??????

Hayo mapungufu ya mama yako ukiyakubali na kumpushi njia sahihi unapungukiwa nini???

Jirekebishe
Penda kwenu
Mheshimu mama yako na wewe utafanikiwa.... eti "anakutawala kijinsia???" Mfyuuuuuuuuu

Ufugaji bora unaweza kuupata kwehye vitabu na uzoefu wa wadau wengine...... tafuta oesa kwanza...hakikisha biashara inasimama vizuri...kisha tafuta chuo karibu na ulipo ambapo unaweza soma hata evening ili uweze kusimamia biashara na kusoma...
 
Kwanza kama mama yako kakusomesha mpaka F6 na uandishi wenyewe ndo huu unaonekana ni kilaza..... tunategemea F6 apange maneno yake kwa umakini.... na huo ukilaza wako unakufanya uone mama yako sio responsible wakati tatizo ni lako zaidi.... kila binadamu ana mapungufu na yawezekana hayo unayo yaona kwa mama
yako yeye anayo ona kwako ni mengi tu.... hakuna kama mama, mvumilie, mwelewe na
mfanye rafiki yako zaidi.... pambaneni kwa pamoja maana uko hapo ulipo sababu yake.... kifupi, nakuona kama unadhani pesa ndo kila kitu, unadhani pesa inaweza kuwa mbadala wa mama
yako, hicho hakiwezekani .... wazo lako la kusomea ufugaji ni jema, wakati unaendelea
kujipanga, anza huo ufugaji mdogo mdogo kwenye kiwanja ulicho nunua kuongeza kipato.... soma na fanya search kwenye Internet kuna mengi tu kuhusu ufugaji, tafuta wataalamu wa ufugaji wakushauri wako wengi tu.. .. mwisho,
mama yako hana mbadala.... mvumilie na
utakuwa nae daima milele mpaka siku za mwisho....
 
Kichwa chako sio smart, ni BRN Fulani hivi. Uandishi wako ni mbovu hauna tofauti na std seven. Sioni point ya wewe kulalamika Ila ninachokiona unapungukiwa critical thinking na kuchanganua mambo. Msaada tu muombe Mungu ili upate akili zaidi
 
Ndugu yangu kwanza mama hana kosa dunia nzima tambua hilo,mimi sijakaa na mama toka nikiwa la tano mpaka sasa nina maisha yangu ,nilikua naishi kwa ma mkubwa later hostel shulen na mpaka vituo vya kulea watoto yatima nimeishi ,mwanzon nilikua namuona mama mkosaji ila sasa natambua kufariki kwa mzee wangu nikiwa la 5 kulimchanganya sana kichwa na nampenda mama yangu kuliko chochote na sasa narudisha fadhila kwa furaha yote ,mama ni mama huwezi jua mangapi anayapitia ndg ukikua ukawa na maisha yako utayafahamu ,maisha ni magumu tambua hilo hakuweka kochi sawa ila mangapi kafanya kukusomesha bado unaweza kuta ana ndugu kawasaidia pia inshort usimlaumu mama na suala la pesa akupe asikupe bado zako utampa sababu kukuleta tu dunian hakuna kikubwa kama hicho.
Suala la chuo nenda kasome ndugu ,mimi niliacha kazi nalipwa laki sita kwa mwezi na hapo nina mke na mtoto nikaenda kusoma kilimo hapo tengeru miaka miwili na sasa sijutii na nimemaliza mwaka jana tu,kasome kilimo (horticulture Tengeru) hutojutia mifugo kwa sasa ajira sio nyingi serikalin ,kilimo private nyingi so hata serikalin wakiwa kimya unaenda kwenye miradi mm nimemaliza mwaka jana ila mpaka leo serikali haijatoa ajira ila sina shaka wala siwazi kwenda huko maana niko private ndg ,fanya uamuzi sahihi kasome ndugu ila somea fani unayojua itakupa maisha na sio ukimaliza uanze kuzunguka na bahasha ,yangu ni hayo usiache kujipanga ada kilimo kwa mwaka ni laki tano tu ,kilimo kasome special kozi zake utafaidi zaidi ambazo ni horticulture -arusha ,irrigation -mbeya na mechanization -tanga
 
Kaa chini na mama yako mjadili kuhusu hayo yote. Unalalamika katumia 3m kati ya 13m? Labda ingekuwa 10m kati ya hizo. Vijana wa arusha mnamatatizo hamjitambui kabisa
 
weee kijana tena unatakiwa umwombe bi Mkubwa msamaha kwa maandishi.;

Hujui thaman ya mzazi weweeee. ukikua utajua
 
Sipendi kuingia sana kwenye suala lako au nianze na SAMAHANI kama ntakua nimeongea kupitiliza, Kwanza kumbuka
Hakuna kama MAMA, hata awe chizi ndioo mwenyezi mungu ameshakujalia MAMA mzuri daima atakua wa mwenzio
kumbuka kua amekulea serekali ilikusomesha baada ya yeye kukufundisha kuanzia kula kuka,kutamba,mpaka kutembea,
hukuamka tuu ukawa na akili zako timamu,hivyo vijipesa unavyoviita sio neno zuri i can undestand kua umekasirika
lakini ndio bahati yako kumpa mzazi kama huyo sasa basi kama alivyokuchukulia mapungufu yako na yeye pia mchukulie
na usimuangaze eti kwasababau ana hela hataki kukupa sio kweli mama kwa mtoto wake anaimani,nenda kwa unyenyekevu
mueleze kwa upole mueleweshe kwa mapenzi niamini atakupa,nakwambia hivyo sababu mimi pia ni mama nilikua na mama pia ambae nimkali sana lakini I use to win her Heart everytime,
kwanza wewe mtoto wakiume tena mama kwa watoto wao wa kiume huwaambi,sasa ebu punguza hasira nenda kaonge nae pole pole na muombe mungu kabla hujaanza kuongea nae akupe subra yakuweza kuhimili iwapo atasema jambo litakukera..
 
Nmepitià shaul zilizotolewa zko sawa km unaakil vzr zifanyie kaz nyongeza usifuge nguruwe tafadhal ufugaj wako utawin.
 
Unaonekana hujajua jinsi ya kudeal na Bi MKUBWA wako;
1. Upo ww na Bi MKUBWA tu sasa shida ni nn? Pangekua na mtu wa kati wa kuintefear hapo sawa.
2. Mpe bi MKUBWA ushauri akikuelewa poa asipokuelewa kaushia.
3.Stand alone, Fanya mambo mengine bila yy.
4. Tafuta kwanza economic stability ili ukiingia school usishake sana.
5. Mshukuru Mungu Kwa ulipifikia. Songa mbele acha kumlaum mama yako. Tafuta fursa zngne pigana kiume utachomoka tu
 
Unaonekana hujajua jinsi ya kudeal na Bi MKUBWA wako;
1. Upo ww na Bi MKUBWA tu sasa shida ni nn? Pangekua na mtu wa kati wa kuintefear hapo sawa.
2. Mpe bi MKUBWA ushauri akikuelewa poa asipokuelewa kaushia.
3.Stand alone, Fanya mambo mengine bila yy.
4. Tafuta kwanza economic stability ili ukiingia school usishake sana.
5. Mshukuru Mungu Kwa ulipifikia. Songa mbele acha kumlaum mama yako. Tafuta fursa zngne pigana kiume utachomoka tu
 
Back
Top Bottom