Mi naona hayakuhusu waache waendelee hilo ni bomu litalipuka tu,ila kaa mbali na huyo jamaa vunja urafiki nae.
mwite mwambie
jamaa akigundua atajua mlikuwa mpo njia moja kumbe wewe aukupendezwa pia na mambo zao
mwite mwonye mwanaume kwa wakt wake...mwite mwonye mwanamke kwa wakat wake.
wakikaidi basi fanya jitihada za kumchoresha ANAYEIBIWA ajue kwamba anaibiwa ili ujivue na LAWAMA ZAO..
Ndugu wanajamvi heshima kwenu.
Ndugu wanajamvi naombeni ushauri juu ya jambo hili ambalo limekuwa kama mzigo kichwani kwangu. Nina rafiki zangu wawili mmoja anafanya biashara za kusafiri na huyu mwingine anafanya kazi hapa hapa Dar kitengo fulani kule bandarini. Huyu mwenzetu anayesafiri ameoa sisi wawili ni Bachelors. Lakini kuna kitu nimekigundua hivi karibuni, huyu rafiki yangu anayefanya kazi bandarini ameanzisha uhusiano na mke wa yule mwenzetu ambaye anasafiri na wote wawili yaani yule mwanamke na yule wa bandarini wameshajua kuwa nimewagundua. Najihisi kumchukia huyu rafiki yangu wa bandarini, namchukia mpaka nakosa raha lakini sijui nifanye nini! kama kuna umuhimu wa kumweleza yule rafiki yangu mwenye mke au vinginevyo naomba mnishauri ndugu zangu.
Liz unajuwa wazinzi au unawasikia tu,huyo jamaa akienda kusema kwa hubby mke atadai huyo jamaa alimtaka akamkataa ndio maana kaja na maneno haya,ni kukaa mbali nao tu bomu litalipuka tu.Ongea na huyo jamaa mwizi kwanza umkanye...mwambie kabisa akiendelea utamwambia rafiki yako anayeibiwa!!!
Huyo mwenye mke kama ni rafiki yako wa kweli then umwambie hata kama utaonekana mbaya!Ni bora sasa hivi kuliko akija kugundua ulikua unajua hukumwambia mpaka akajua kwa namna nyingine!!!
Dah! huyo mwanamke amekosa wanaume! adi aje kutembea na huyo rafiki w mume wake ....mke wangu nikikuta anatembea na rafik yangu naua bora nikute ni m2 nicyemfahamu.