Naombeni msada: Nahitaji kuonana na Rais Samia

Azimio la kazi

Senior Member
Joined
Jun 7, 2023
Posts
138
Reaction score
452
Wakuu habarini,

Niende kwenye mada moja Kwa Moja, Wakuu naomba msaada nahitaji kuonana na Rais Samia Suluhu Hassan na jambo muhimu sana natamani ni mwambie physically. Ikishindikana basi nionane na waziri mkuu ndugu Kassimu Majaliwa Kassimu.

Lakini sifahamu utaratibu na namna ya kuonana na hao wakuu

Naombeni muongozo.

===

 
Nenda kwa mtendaji wa serikali yako ya Mtaa ama ya Kijiji atakupa utaratibu mzimab bila kutozwa toza ana Kodi ya namna yoyote. Rahisi sana.
 
Kwani hana Sekretari? Basi pitia kwa msemaji wake wa Serikali, mpatie malalamiko yako kisha atayafikisha ama tumia email ya Ikulu.
 
Sema shida yako hapa kwa ufasaha atafikishiwa ila
Usidanganywe kwamba utaonana nae kirahisi tu kama kuonana na classmate wako. Vinginevyo kafanye kituko kimoja kwenye mkutano wake wa hadhara labda atakuona akusikilize una shida gani, kabla polisi hawajakutupia kwenye defender kama mzoga.

 
Naskitika Ndugu yetu tunaenda kumpoteza... Acha kabisa mkuu... muulize #CkAllan wa #MadamPresident
 
Andika BARUA CHAP...... Kwenye hiyo barua mwandikie linalokusibu na uweke namba zako za simu zinazopatikana muda wote....... Mwandikie yote kwa kirefu
 
Umesema ni siri sawa ila tuambie walau dondoo jambo linahusu nini
Je ni ishu ya uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya ofisi umeyagundua?
Je ni wewe umetendewa jinai hivyo unahitaji haki yako ambayo unahisi level za chini hutasaidiwa?
Je ni ushauri wa masuala ya kiuchumi?


Funguka mkuu walau intro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…