fundiaminy
JF-Expert Member
- Jun 4, 2009
- 354
- 52
Kwa mazingira uliyoyaeleza mi nashauri huyo baba atafute kuwakutanisha na kuwapatanisha hao wamama wawili. Kisha wapange zamu ya kuwa na mzee, halafu mzee awe transparent kuhusu mapato kwa wote wawili na kila mmoja apate mapenzi na huduma sawa. Kama inawezekana
Huyo mama wa nyumbani wa darasa la saba utamuonea ukitaka aanze kusoma sasa hivi. Ukitaka mzee amwache bimdogo nayo nahisi itakuwa ngumu. Bimdogo kumuacha mzee nayo inaweza kuwa ngumu.
Ni mawazo yangu tu
Salamu kwenu nyote Mabibi na Mabwana, natumaini mko Salama kabisa.
Kuna jambo moja nimeliona likanipa maswali mengi, halafu nikawa sipati majibu mazuri.
Kuna ndoa moja ya mume moja na mke mmoja wote Wakristo. Sio ndoa changa wanandoa ni watu wazima kabisa. Kwenye miaka ya 50's hivi.
Baba ana elimu kubwa ni mfanyakazi na mfanya biashara pia.
Mama/mke wake wa ndoa ni mama wa nyumbani, hakubahatika kupata Elimu ya juu, tuseme ana Elimu ya msingi.
Baba huyu ana mpango wa kando (Mke mwingine nje ya ndoa) na amezaa naye mtoto mmoja. Kilichonipa maswali sasa ni kwamba huu mpango wa nje walau umeenda shule, unajua mambo hasa yahusuyo biashara na maisha kwa ujumla.
Huyu mama mwenye nyumba (mke wa ndoa) yeye ni mama wa nyumbani pure!!
Anashinda nyumbani, anaangalia tu taratibu za hapo nyumbani.
Mipango mingi inayohusu maendeleo ya biashara na maisha kwa ujumla, Baba anapanga na huo mpango wa kando, kila kitu lazima mpango wa kando ahusishwe na atoe maoni yake.
Na huo mpango wa kando unajua mambo, kufikiri, na maoni na ushauri mzuri wa kimaendeleo. Ambacho nimekigundua mpango wa kando unajua kufikiri kuliko mpango wa ndani. Yani ukimsikiliza huyo mpango wa kando na mother house katika kutoa hoja na kuchangia jambo lolote la maendeleo unagundua kabisa kuna gape kubwa la uelewa wa mambo, wakati mwingine hata utendaji wao.
Na hicho kimepelekea baba kuelemea zaidi huko kwa mpango wa kando kwa sababu huko ndiko anakopata Innovative ideas zaidi.
Ingawa analala na kukaa nyumbani kwa mke wake wa ndoa. Kiukweli ukiangalia unaona huyu mpango wa kando ana mchango mkubwa sana kwenye maswala ya maendeo ya kiuchumi zaidi kuliko mother house.
Kuna wakati huyo baba alimfungulia mother house wake biashara kubwa na nzuri tu, lakini alishindwa ku manage ikafilisika kabisa.
Lakini kuna viyu huyu mpango wa kando anaviangalia vinakwenda vizuri sana, na vina leta faida kweli kweli.
-Kama ilivyo kawaida mother house hana furaha na kile anachokifanya mume wake, kumletea hadi mtoto kwenye ndoa. Hana ujasiri kwa mume wake, ni mnyonge, hana maamuzi yake binafsi, hana uhuru wa kutosha. Yani ni tabu tupu. Anaishi tu kwa sababu kuna kuishi lakini hana furaha ya ndoa kabisa. Na kwa sababu ya hayo anazidi kuwa kituko kabisa, hata house girl anaweza akamfokea!!
1.Je huyu baba alikosea kumuoa mke ambaye hana kiwango cha elimu zaidi ya
elimu ya msingi??
2.Je kwa nini huyu baba asimwendeleze huyu mama/mke wake kielimu
kidogo ili aweze kuchangamsha akili kidogo?
3. Je ni vizuri mtu kuoa/kuolewa na mtu ambaye walau akili zenu zinaendena katika utendaji wa mambo hasa ukizingatia mipango na maono yako ya maisha?
4. Je huyu baba anafanya makosa kumfanya mpango wake wa kando
mshauri wa mipango yake ya maendeleo zaidi ya mke wake?
Mwisho: Unamshauri nini huyu mama mwenye nyumba, ili aweze kuishi kwa furaha na amani katika ndoa yake?
Mbarikiwe!!!
Yani Michelle tuko pamoja kabisa, ndo maana nimesema hili jambo limenipa utata,
Kwa sababu ukiangalia huyu mpango wa kando ana kila sababu ya kuendelea kubaki na huyu baba, yani ana efect kubwa sana kwenye maendeleo ya uchumi wake. Lakini sasa?? Hiyo ndoa hiyo, ilikuwa au ni wrong ndoa??
Ok, unajua kuna akili nyingine ipo vile ilivyo, hata ukiipa majibu ya mitihani inaweza ikafeli vile vile?
Hawa wanandoa walikosea wapi hasa?
Thanx Michelle haya mambo mamiangu yaache tu............... ni magumuNapenda sana MJ1 waga unafikiri kwa mapana na marefu.....i admire that....
Unajua mimi nina amini kuna watu hawakupaswa kuoana,yaani pengine circumstances ziliwaweka pamoja,hasa hizo ndoa za zamani....sasa huyu baba kakutana na soulmate wake haswaaa na mambo ndo yamekuwa hivyo......maisha haya.....
Aisee nlikuwa sijaisoma thread vizuri:
Siku nyingine LD uwe unaandika maneno machache bana!
Will be right back
Msimamo wa babu ambao ndio hali halisi na ukweli ni huu:
Mwanaume hajawahi na wala hatakaa aridhishwe na mwanamke mmoja
Mwanaume hajaumbwa kwa ajili ya mwanamke mmoja.
Mama mwenye nyumba hana alichokosea....hata angekuwa na upeo sawa na mumwewe, ameenda shule kama mumewe, angekuwa mjasiriamali mzuri, mzuri kama Cleopatra....bado jamaa angetoka nje.....(mwanaume haridhiki kuwa na mwanamke mmoja, msisahau)
Baba kuwa na mpango wa nje pia hajakosea.....kwa kuwa hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke mmoja.
Alichokosea huyu bwana:
Kuzaa nje ya ndoa....kama mkewe hana shida ya uzazi kilichompeleka kutotoa huko nje ni nini?
Kumdharau mke wake.....Ameshindwa nini kufanya mpango wa nje kwa siri?
Kuuachia mpango wa nje kuendesha biashara zake....Likiingia limbwata hapo, au mzee akaRIP ghafla vilio vya watoto wake wa mpango wa ndani vitamlilia mpaka jehanamu atakapokuwa.
Huu ni msimamo wa babu na hauusiani na imani ya dini yoyote ya dini wala mashirika ya kutetea jinsia za watu!
Duh Babu............ama kweli Mwacheni Babu aitwe Babu.............Ye wa kwanza kuliona jua bana.
Msimamo wa babu ambao ndio hali halisi na ukweli ni huu:
Mwanaume hajawahi na wala hatakaa aridhishwe na mwanamke mmoja
Mwanaume hajaumbwa kwa ajili ya mwanamke mmoja.
Mama mwenye nyumba hana alichokosea....hata angekuwa na upeo sawa na mumwewe, ameenda shule kama mumewe, angekuwa mjasiriamali mzuri, mzuri kama Cleopatra....bado jamaa angetoka nje.....(mwanaume haridhiki kuwa na mwanamke mmoja, msisahau)
Baba kuwa na mpango wa nje pia hajakosea.....kwa kuwa hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke mmoja.
Alichokosea huyu bwana:
Kuzaa nje ya ndoa....kama mkewe hana shida ya uzazi kilichompeleka kutotoa huko nje ni nini?
Kumdharau mke wake.....Ameshindwa nini kufanya mpango wa nje kwa siri?
Kuuachia mpango wa nje kuendesha biashara zake....Likiingia limbwata hapo, au mzee akaRIP ghafla vilio vya watoto wake wa mpango wa ndani vitamlilia mpaka jehanamu atakapokuwa.
Huu ni msimamo wa babu na hauusiani na imani ya dini yoyote ya dini wala mashirika ya kutetea jinsia za watu!
1.Je huyu baba alikosea kumuoa mke ambaye hana kiwango cha elimu zaidi ya
elimu ya msingi??
2.Je kwa nini huyu baba asimwendeleze huyu mama/mke wake kielimu
kidogo ili aweze kuchangamsha akili kidogo?
3. Je ni vizuri mtu kuoa/kuolewa na mtu ambaye walau akili zenu zinaendena katika utendaji wa mambo hasa ukizingatia mipango na maono yako ya maisha?
4. Je huyu baba anafanya makosa kumfanya mpango wake wa kando
mshauri wa mipango yake ya maendeleo zaidi ya mke wake?
Mwisho: Unamshauri nini huyu mama mwenye nyumba, ili aweze kuishi kwa furaha na amani katika ndoa yake?
Mbarikiwe!!!
Asante babu yangu,
Lakini sasa babu, mbona akili yangu inakataa kuamini kwamba wanaume wote lazima watoke nje ya ndo?
Kwani wanaume hawafuati sheria na amri za Mungu?
Muhosni wako ni ushauri mzuri sana huu ninakubaliana na wewe ila nina mashaka
1. Utakapowakutanisha na kuwaeleza ukweli juu ya mapato ya familia- Bimdogo anawezaanza kuleta dharau kuwa yeye ndo anayeendeleza familia na kumfanya bi mkubwa ajinyongee......
2. Hata bila kuletewa dharau, kitendo tun cha kumweleza Bi mkubwa kuwa - mafanikio yote yameletwa na huyu mwenzio ni sawa na kumwambia yeye ndoa hakuiweza.......
Nadhani Baba atafute ustaarabu wa kuinua confidence ya Bi Mkubwa hata kama ni kumpeleka kwenye vikozi vya Biashara.
N.B Hakuna ukomo wa elimu Muhosni kwa elimu yake ya darasa la saba am sure hawezikosa kikozi kitakachomsaidia ujuzi hata wa biashara ya kuunguza Batiki