Naombeni msaada wanasheria tafadhali

ladyfocus

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
946
1,000
Nitatoa story kwa ufupi ilivyokua, nilimkopea mtu pesa kwenye kikundi zaidi ya milioni kumi, baadae akakimbia na ndugu zake wakaahidi kulipa kwa kusema kuwa Mimi nilipe huko kikundini then wao watalipa ila tuwape muda. Nikajilipia lile deni na tukawapa mwaka mzima walipe. Mwaka ukakata siku ya makubaliano ikafika hawakulipa.

Tukaenda mahakamani wakakataa kuwa siwadai wao ila ndugu yao na hawajui alipo nadhani na rushwa ikatembea wakashinda kesi kwa point kuwa wao si wadaiwa halisi.

Je, naweza kumfungulia huyo aliyetoroka kesi ya wizi wa kuaminika na nikawabana ndugu zake wamfichue alipo coz wanamficha?

Naombeni ushauri wowote au msaada. Nipo Arusha
 
rikiboy

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
13,546
2,000
Ulifanya Kosa kubwa sanaa KULIPA HIZO PESA kwa niaba ya jamaa.. Kama alikuwa ni member wa kikundi hiyo ilibidi iwe hasara ya kikundi sio ya mtu binafsi.

Pole lakini hapo huna chako na hao ndugu huwezi wafanya chochote maana hamna ushahidi hata wa maandishi kuonesha makubaliano zaidi ya maneno tupu. Pole sana
 
MoneyHeist4

JF-Expert Member
Jul 10, 2017
932
1,000
Mkuu pole sana hapo ushapata hasara ya milion 10, hao ndugu huwezi kuwafanya chochote maana hawahusiki na chochote juu ya hizo pesa.

Sasa hivi simwamini binadamu yeyote kwenye swala la pesa bora lawama kuliko fedheha.
 
ladyfocus

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
946
1,000
Ulifanya Kosa kubwa sanaa KULIPA HIZO PESA kwa niaba ya jamaa.. Kama alikuwa ni member wa kikundi hiyo ilibidi iwe hasaraa ya kikundi sio ya mtu binafsi. Pole lakini hapo huna chakoo na hao ndugu huwezi wafanya chochote maana hamna ushahidi hata wa maandishi kuonesha makubaliano zaidi ya maneno tupu. Pole sana
ushahidi wa maandishi ulikuwepo na ndio tuliupeleka mahakamani
 
Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
15,351
2,000
Nitatoa story kwa ufupi ilivyokua, nilimkopea mtu pesa kwenye kikundi zaidi ya milioni kumi, baadae akakimbia na ndugu zake wakaahidi kulipa kwa kusema kuwa Mimi nilipe huko kikundini then wao watalipa ila tuwape muda....
Je, kuna mahali mliandikishiana na hao ndugu walipo ahidi kulipa?

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Ndekrepha

JF-Expert Member
Jun 4, 2020
1,496
2,000
Huyo ndugu yao aliejificha ulipomkopesha hizo hela mliandikishana? Kuna ushahidi wa kuonesha kwamba ulimpatia hizo milioni 10? Hao ndugu waache kwanza na huo mkataba uliosaini nao uhifadhi.

Tumia njia yoyote kupata contact za huyo ndugu yao aliekimbia, msake kwa kutumia hata watu wa mitandao ya simu. Tumia fedha kidogo na wewe. Ukimpata bhas mfikishe tu sehemu ya sheria hao ndugu zake ndio watakuja kumtoa na kumlipia.
 
duuh kupata contact ni hadi hao ndugu zake watoe, ule mkataba upo mahakamani ulitumika kama ushahidi, naweza kufanyaje hapo?
 
Ndekrepha

JF-Expert Member
Jun 4, 2020
1,496
2,000
duuh kupata contact ni hadi hao ndugu zake watoe, ule mkataba upo mahakamani ulitumika kama ushahidi, naweza kufanyaje hapo?

Dah mkuu inaonekana haupo serious ndio maana wanakuzungusha hao watu. Hukutoa kopi huo mkataba? Anyway kama uko mahakamani bhas sio mbaya utakuwa uko filed kwenye jalada. Unawezekana kupatikana tena kwa marejeo.

Huyo mtu kama uliweza kumkopesha kiasi kikubwa hivyo cha pesa it means ni mtu unaemfahamu, unaijua circle yake vizuri hivyo tafuta njia yoyote ya kutafuta contacts zake kupitia circle yake, ndugu waweke pembeni kabisa wala usiwaombe wala kuwajulisha kama unamtafuta huyo ndugu yao. Mtafute kimya kimya kwa kufatilia kwenye circle yake.
 
IPO hivi mkuu huyu mtu zaidi ya hao ndugu zake sina watu wengine ninaowafahamu na utawezaje kiwaaproach wakupe contact zake na wanajua ishu nzima? Nilikua nawaza siwezi kuwakamata kwa kosa la kuficha mhalifu then wakamtoa alipo?
 
Ndekrepha

JF-Expert Member
Jun 4, 2020
1,496
2,000
IPO hivi mkuu huyu mtu zaidi ya hao ndugu zake sina watu wengine ninaowafahamu na utawezaje kiwaaproach wakupe contact zake na wanajua ishu nzima? Nilikua nawaza siwezi kuwakamata kwa kosa la kuficha mhalifu then wakamtoa alipo?

Mkuu, i`m sorry nimesema hauko serious na ninaweza kurudia tena hivyo kuwa hauko serious ndio maana wanakusumbua. Kwani hao ndugu zake ni lazima uwa approach wewe? Huyo mtu ulimkopesha fedha za nini? Ni za biashara? huna watu unaowajua ambao alikuwa anafanya nao shughuli zake? Tafuta circle ya huyo mtu, watu aliokuwa anajihusisha nao kama ni kazini au kwenye biashara. Hao ndugu zake wanaku monitor kila move unayofanya ndio maana wanajiamini.. na wewe wazunguke kwa kufuata circle yake bila kuwahusisha ndugu.. tumia watu baki kufatilia hilo na kutafuta hizo contact na wafanye communication wewe ni kuandaa tu RB yako wape watu hiyo kazi watafanya. Huna uchungu na hiyo hela wewe..ungekuwa ushampata haraka sana.
 
daah I wish ungejua mazingira, hatahivyo nashukuru sana kwa kujali. Ngoja niendelee kukusanya ushahidi nijue naanzia wapi tena
 
Ndekrepha

JF-Expert Member
Jun 4, 2020
1,496
2,000
daah I wish ungejua mazingira, hatahivyo nashukuru sana kwa kujali. Ngoja niendelee kukusanya ushahidi nijue naanzia wapi tena
Kila la kheri mkuu, nenda kituo cha polisi utoe maelezo yote kwa ufasaha ya mchakato wote. Utapewa mtu wa kufatilia hiyo kesi naamini huyo jamaa atapatikana tu na muafaka wa hilo deni lako utafikiwa.
 
sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
814
1,000
daah I wish ungejua mazingira, hatahivyo nashukuru sana kwa kujali. Ngoja niendelee kukusanya ushahidi nijue naanzia wapi tena
Pole sana mkuu, hii ndio dunia.

  1. Kesi uliyomshtaki hao ndugu iliisha lini? na je ilikuwa ni hukumu ama uamuzi (decree or ruling)?
  2. Ilikuwa ni kesi ya nini (madai, jinai nk)?
  3. Maandishi mliyoandikishana na ndugu, walitamka chochote kuhusu ndugu yao? kama kutaja jina kamilifu la huyo mtoro

Google the Doctrine of Estoppel, itakusaidia dhidi ya hao ndugu hata kama ni kwenye rufaa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom