Naombeni msaada wa ushauri nasaha


Hapo kwenye baraza la wapatanishi ndio penye tatizo...hivi kweli watu mmetengana miaka miaka miwili, no feelings anymore, pengine mnachukiana...kuna upatanishi hapo!? Na kama hatutaki kupatana, tunataka kuachana kila mmoja ashike hamsini zake bado hao wanabaraza watapoteza time yao kuwapatanisha...ooops, they are paid to waste their time au siyo!

Kwa nini mwanamke anayenyanyasika hasiweze pata talaka na stahiki zake akaishia zake huko kuendelea na maisha yake!
 
Mhmmm!!! Ngoja nikae pembeni niwaachie wana sheria wamwage point zao.
 
Hizi ndio taratibu zilizo wekwa mkuu Riwa! Lazima baraza lijilizishe kuwa hii ndoa haiwezi kuendelea ndio taratibu za kufile devorce zianze! Na huwezi kupata haki ya kupewa talaka kama hujapitia hapo! Na haya mabaraza yapo kuhakikisha ndoa hhazivunjwi bila sababu za msingi maana wanacho fanya ni kujaribu kuokoa ndoa!

Sasa hapo kwenye kutengana miaka miwili ndio sababu huyo dada ana takiwa kwenda nazo ili kuhakikisha ndoa inavunjwa,maana na hapo hawshiriki tendo na kama alikuwa ana nyanyaswa hayo yote atayaeleza kule ili wao waone hii ndoa imeshindikana, kumbuka na mwanaume atakuwepo kujitetea!
 
Last edited by a moderator:
Hapa njia ya yeye kutumia ni ya kupitia ustawi, japo huyu jamaa ana hofia kupoteza mali.

Hapa huyu dada ajipange vizuri hata kama jamaa atakuja na sababu kuwa tulitengana maana alikuwa ana nisaliti lakini bado nampenda na niko tayari kurudiana nae!
Na kwa swala la kumtuhumu kumsaliti linaweza likakosa nguvu pengine jamaa hana ushahidi!
Mdada akisisima hapo kwenye separation 2years na ikaonekana tuhuma ya kusaliti haikuwa kweli basi hiyo itakuwa sababu tosha ya ku file devorce!

Tatizo la jamaa hapa ni hizo mali

 
Pole nyngi kwa dada yetu ...
Pia anaweza pata msaada kwa Albedo
 
Last edited by a moderator:
kila mahali keshapita,anataka kujua kesi kama hii kisheria imekaaje mkuu
mi nipo pouwa
legally speaking huyo mdada anazo grounds za kutosha za kupata haki yake lakini kitu anachotakiwa kujua kwamba mahakama za Tanzania hazipendelei kuvuja ndoa..inabidi hiyo ndoa ifikie stage inaitwa broken down irrepairable...halafu vile vile kesi hizi zina tendency ya kuchukua muda mrefu 4-8 yrs hivi...
 

Daktari huo ndio utaratibu wa kisheria. Kuna wanandoa wanaweza kupatanishwa katika mabaraza ya upatanishi wa ndoa na kuishia hapo. Ila wapo wasiopatanishwa kutokana na mazingira ya ndoa yao au tofauti zao katika ndoa.

Mtu hawezi tu kuanzia mahakamani kufungua madai ya talaka. Mahakama lazima itauliza kama wanandoa wamejaribu kupitia hatua za upatanishi na katika hatua hizo wameshindwa kupatana. Na kama wameshindwa kupatana lazima uoneshe certificate inayosema hivyo ili uendelee na hatua zaidi kimahakama. Hata hapo mahakamani, Mahakama itakuambia hatupo hapa kuvunja ndoa, hivyo lazima wathibitishe kuwa ndoa husika hairekebiki/imevunjika au mazingira ya wanandoa husika yamesababisha ndoa kuvunjika pasipo kurekebika. Hapo ndio wanatoa hati ya talaka na oder nyingine kama za mgawanyo wa mali ya wanandoa.
 

Nadhani Smile utakuwa amepata muongozo wa kumsaidia mdada.
 
Last edited by a moderator:
mwanaume alimshutumu wife kutokuwa mwaminifu akamfukuza bila hata nguo,na kagoma kumrudisha hadi leo.
Nadhani uthibitisho huo unamtosha aende tu mahakamani akadai talaka.

Wanaume wengi vichaa sa kama hamtaki mke na anaogopa kumpa mali anauhakika gani ataishi na mali hizo...sijawahi kusikia mtu mdhulumaji akatajirika isipo kuwa kwa mda tu, afu anarudi umasikini kuliko alio kuwa nao mwanzo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…